MAKALA
OUR EVENTS
MBINU ZA MAFANIKIO
CHANGAMOTO NA TIBA YAKE
Thursday, April 18, 2019
Saturday, February 4, 2017
MWENYEKITI WA BODI YA WEZESHA TRUST FUND MZEE ODILO TWEVE ALIPOFANYA KIKAO CHA MIEZI MITATU NA WAFANYAKAZI WA WEZESHA TRUST FUND - OFISINI SABASABA MOROGORO
Wezesha Trust Fund ina kawaida ya kufanya vikao mara kwa mara na Mwenyekiti na wakuu wa Bodi yake ili kujadiliana kuhusu maendeleo na mustakabali wa Asasi hii. Mwezi wa Saba, 2016 Mwenyekiti wa Bodi ya Wezesha Mzee Odilo Tweve alifanya kikao kujadili jinsi ya kufikia malengo yaliyowekwa na kukumbushana wajibu wa kila mfanyakazi wa Wezesha.
Mungu ni mwema kikao kilienda vizuri sana na majukumu yalifanyika kwa ufasaha sana, na maandalizi ya kutimiza miaka minne ya Wezesha yalipangwa na kuhakikishwa kuwa yatatimia katika mustakabali uliowekwa.
Pichani hapa chini ni Mwenyekiti pamoja na wafanyakazi wakijadiliana kwa kina kuhusiana na Asasi hii.
Mwenyekiti Mzee Odilo Tweve akiongea kwa msisitizo mambo kuhusu miaka minne ya Wezesha Trust Fund nini kifanyike na kifanyike kwa namna ipi, wafanyakazi wakimsikiliza kwa weledi na utulivu mkubwa.
Mzee Boniface Mbogo nae ni mjumbe wa Bodi ya Wezesha Trust Fund akisikiliza kwa makini na akitoa hoja zenye mashiko makubwa kuhakikisha kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa. Abuu Mkingie mratibu wa mambo ya nje akitoa hoja zake za kuhakikisha atazungukia kila mahali kuweka sawa mambo yaliyopangwa kwa uweledi.
Mungu ni mwema kikao kilienda vizuri sana na majukumu yalifanyika kwa ufasaha sana, na maandalizi ya kutimiza miaka minne ya Wezesha yalipangwa na kuhakikishwa kuwa yatatimia katika mustakabali uliowekwa.
Pichani hapa chini ni Mwenyekiti pamoja na wafanyakazi wakijadiliana kwa kina kuhusiana na Asasi hii.
Mwenyekiti Mzee Odilo Tweve akiongea kwa msisitizo mambo kuhusu miaka minne ya Wezesha Trust Fund nini kifanyike na kifanyike kwa namna ipi, wafanyakazi wakimsikiliza kwa weledi na utulivu mkubwa.
Mzee Boniface Mbogo nae ni mjumbe wa Bodi ya Wezesha Trust Fund akisikiliza kwa makini na akitoa hoja zenye mashiko makubwa kuhakikisha kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa. Abuu Mkingie mratibu wa mambo ya nje akitoa hoja zake za kuhakikisha atazungukia kila mahali kuweka sawa mambo yaliyopangwa kwa uweledi.
Friday, January 20, 2017
WEZESHA TRUST FUND WALIPOFANYA ZIARA KWA WAHANGA WA MAFURIKO WILAYA YA KILOSA MEI, 2016
Wafanyakazi wa Wezesha Trust Morogoro walipotembelea Wilayani Kilosa kuwapa pole wahanga wa mafuriko Wilayani Kilosa. Mafuriko hayo yalitokea mwanzoni mwa mwaka 2016. Wezesha ilitoa pole kwa misaada ya nguo, chakula na pesa taslimu. Pia Wezesha walienda kuangalia eneo lililoathirika na mafuriko kijijin na mto wa Tindiga ambao ni chanzo cha mafuriko.
Watoto walioathirika na mafuriko wakiwa wanacheza eneo la tukio kwani imekuwa kama jangwa, mazao yalipotea, mkondo wa maji umeharibu shule, makanisa na hata sehemu za watoto kucheza.
Wamama waliothirika na mafuriko wakiwa wanatoka kuchota maji mbali na makazi yao, kisima cha maji kilizibwa na matope makali na ikafikia mahali maji yalikuwa shida, lakini Mungu ni mwema wameviona baadhi ya visima na wanaendelea na maisha mahali hapo.
Wezesha Trust Fund inawaomba watanzania, wanajamii na wadau wote kwa ujumla kujitoa kwa uadilifu katika kila janga linalowapata wenzetu. Jamii yetu ni wamoja tupendane na kutendeana yaliyo mema na Mungu wa Mbinguni atatulipa.
Mkurugenzi wa Wezesha Trust Fund Bi Lusako Mwakiluma akikabidhi misaada kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mheshimiwa Henjewele Mei, 2016, misaada iliyokabidhiwa ni chakula, nguo, fedha taslimu na vitu mbalimbali.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Henjewele akishukuru Asasi ya Wezesha na wadau wote waliochangia hali na mali kuhakikisha misaada inapatikana na kupelekwa Kilosa kwa wahathirika wa mafuriko. Mungu awabariki wote waliotoa kwa upendo misaada hiyo.
Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa wakishusha misaada toka kwenye gari baada ya Wezesha kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kilosa. Aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya aliongoza ushushaji wa misaada hiyo.
Wafanyakazi wa Wezesha Trust Fund walipokuwa Kilosa mara baada ya kukabidhi misaada hiyo kwa Mkuu wa Wilaya kutoka kushoto Mohamed Nyongo(Kaimu Afisa Mafunzo), Janeth Lupupa(Afisa Mafunzo) na Abuubakari Mkingiye(Mratibu wa mambo ya nje) wanaiomba jamii kujitoa kwa hali na mali katika matukio yoyote yanayowahusu watu wengine kwani wanaamini kutoa ni moyo wala sio utajiri.
Wafanyakazi wa Wezesha wakitathmini athari za mafuriko katika nyumba za wenyeji ambao walizikimbia baada ya mafuriko kutokea kutoka kulia ni Mohamed Nyongo(Kaimu Afisa Mafunzo) na Salum Tindwa(Mratibu wa Miradi) Wezesha Trust Fund. Kwa kweli hali ilikuwa ni mbaya lakini Mungu amesaidia wahathirika wako sehemu sahihi kwa muda huu.
Nyumba iliyoathirika na mafuriko ikiwa imeezuliwa paa na uharibifu mkubwa, maji yaliingia ndani ya nyumba kiasi cha 3/4.
Watoto walioathirika na mafuriko wakiwa wanacheza eneo la tukio kwani imekuwa kama jangwa, mazao yalipotea, mkondo wa maji umeharibu shule, makanisa na hata sehemu za watoto kucheza.
Wamama waliothirika na mafuriko wakiwa wanatoka kuchota maji mbali na makazi yao, kisima cha maji kilizibwa na matope makali na ikafikia mahali maji yalikuwa shida, lakini Mungu ni mwema wameviona baadhi ya visima na wanaendelea na maisha mahali hapo.
Wezesha Trust Fund inawaomba watanzania, wanajamii na wadau wote kwa ujumla kujitoa kwa uadilifu katika kila janga linalowapata wenzetu. Jamii yetu ni wamoja tupendane na kutendeana yaliyo mema na Mungu wa Mbinguni atatulipa.
Lusako Mwakiluma
Mkurugenzi
Wednesday, January 18, 2017
JE, UTAWEZAJE KUSHINDA HALI NGUMU YA MAISHA NA AJIRA
MBINU 6 ZITAKUSAIDIA SANA
Kutokana na mabadiliko ya
tabia nchi na hali ya kukua kwa uchumi mambo mengi yamebadilika sana, Hivyo
basi ni muhimu tujifunze njia za kujiimarisha ili tuweze kupita salama katika
hali hii, usipoteze muda kulalamika amka anza kuangalia mbinu hizi ili uboreshe
maisha yako. Nenda na dira usiwe
mchelewaji wah sana uone faida ya kuwa wa kwanza katika kutatua matatizo na
kupata fursa zilizopo karibu uone mbinu ambazo zitakusaidia kuinuka kiuchumi
kwa haraka.
1. Uhuru wa fikra: Kama kuna nyakati ambapo
unahitaji uwezo wa kuiona dunia kama ilivyo na sio kama unavyotaka iwe, basi ni
sasa. Ni muhimu kuboresha ufahamu wako wa mambo mengi ya kimsingi ya kimaisha
kama vile mapenzi, biashara, tabia, teknolojia ,, na zaidi sana maswala ya kiroho.
Uhuru wa kifikra
utakuwezesha uweze kujitawala vema, kwani kimsingi wewe ndiye mtu wa kwanza
kabisa unayeweza kuleta mabadiliko makubwa na maendeleo kwa maisha yako,
kwakuwa unayo nguvu ya utashi, kufanya
maamuzi au kuacha watu waamue mambo kwa ajili yako.
2. Kuboresha mtandao: Kwakuwa unahitaji kutambua fursa
nyingi kwa kadri inavyowezekana na kwa kuwa wewe ni mzalishaji, unahitaji sana
kujenga mtandao mkubwa na mtandao wenye manufaa ili kuweza kutambua fursa
mbalimbali kupitia mtandao wako, na pia kuweza kuuza bidhaa zako kupitia
mtandao huo.
3. Kuwa mzalishaji: Katika machafuko
haya, bidhaa na huduma mbalimbali zitakuwa adimu, na kwa
wazalishaji wachache watakaoweza kuzalisha kwa ufanisi wataweza kujikuta
wakiendesha maisha vizuri. Hivyo pamoja na kuwa
mtumiaji wa fedha zako kwa mambo ya burudani, unahitaji kuhifadhi fedha zako
kwa namna ambayo fedha zako hazitopoteza thamani zake, na wakati huo huo,
ukifanya utafiti wa aina ya bidhaa au huduma ambazo utakuwa ukizalisha, ili
nawe unufaike na mazingira tuliyonayo. Kuendelea kuwa
muingizaji wa kipato (kwa njia ya ajira pekee) na kuwa mtumiaji zaidi ya
mwekaji akiba, si jambo la busara, hasa katika hali ngumu ya kiuchumi na
kijamii tuliyonayo.
4. Kuwa mwepesi wa kubadilika: Mambo mengi yanabadilika
kwa haraka sana, ufahamu uliokuwa nao jana , mbinu ulizotumia siku za nyuma hata kama zilifanikiwa, inawezekana kabisa
zisifanikiwe kwa sasa, na kwa kadri mambo yanavyozidi kubadilika. Ushindi wa
kipekee unakuja pale unapoweza kuwa mwepesi wa kubadilika, kwa kubuni njia mpya
na bora za kukabiliana na mazingira unayokumbana nayo.
5. Kaa tayari kwa kusafiri: Fursa zinaweza kutokea popote pale, hivyo kuwa tayari
kusafiri nje ya mkoa uliopo sasa, na zaidi sana nje ya nchi. Hakikisha una
passport halali na isiyoisha muda wake, na tambua taratibu za kusafiri nje ya
nchi, kama vile mambo ya visa, na gharama
za maisha kwa nchi tofauti.
6. Mipango ya muda mrefu: Tambua kuwa hali
hii ngumu ya maisha ni swala ambalo litaendelea kwa muda mrefu, hivyo ni muhimu
kujipanga wewe na familia yako. Kama una watoto au una mpango wa kuwa na
watoto, basi ni wakati wa kufikiria pia namna ya kuja kuwawezesha watoto wako
wawe na ujuzi wa uhakika, na kuwa wawe wazalishaji. Hakikisha unajitengenezea ujuzi na uzoefu uliokomaa
katika jambo fulani au mambo kadhaa tofauti, ili uweze kuja kuuza ujuzi na
uzoefu wako huo katika soko gumu la huduma tunalokumbana nalo kwa nyakati za
leo na zijazo.
Lusako Mwakiluma
Muhamasishaji na Muinuaji
January, 2017
Sunday, January 1, 2017
SABABU ZINAZOPELEKEA WANAWAKE KUWATEGEMEA WANAUME JAPOKUWA WANA FURSA NYINGI SANA
Fursa za wanawake ziko nyingi sana lakini wanawake wenyewe
hawana motisha ya kuzikimbilia na kwenye uzalishaji mali wako vizuri sana ila
tu kuna baadhi ya wanawake ni waoga kujaribu nab ado wanaamini kuwa mwanaume ni
mtafutaji na mwanamke ni mama wa nyumbani siku zote. Hii inaonyesha mwanamke akiishi bila
mume au akikimbiwa na mwanaume
anashindwa kusimama kwa hofu ya
kushindwa maisha. Kuna fursa za
kibiashara, ufugaji na utengenezaji bidhaa mbalimbali ambazo kila siku
zinajitokeza lakini katika suala la kujifunza wanawake ni wazito na hata
kuuliza kama kitu hawawezi pia ni taabu.
Wezesha Trust Fund inatumia njia nyingi
katika kuwaelimisha wanawake: Inatumia
Television, Redio, semina na warsha za mara kwa mara. Wanawake wengi wanatambua kuwa kila mwanaume aliyefanikiwa
nyuma yake yuko mwanamke na ukikuta mwanamke kafanikiwa ujue nyuma yake yuko
peke yake. Wanawake pia wana majukumu mengi ya kifamilia na ya kibiashara, apike, afue, aende kazini, anyonyeshe na pia amhudumie mume na watoto. Muda wake ni ule ule na kazi ni nyingi, kuna muda anachoka kwani naye ni binadamu.
Wakati naongea na wanawake hawa nakutana na
changamoto nyingi wanazopitia wanalalamika wenyewe kwamba hawajiamini, waoga,
na wakiona biashara kidogo zinasumbua wanaacha.
Na kuna wengine mitaji inakata kwa sababu ya waume zao wanawaachia
majukumu ya nyumbani na pia wanaume hao hao hawawapi fursa wanawake zao za
kufanya biashara kwa upana zaidi. Pia wengine wanawakataza wasitoke majumbani
kwenda kwenye biashara. Wapo wanawake
wengine wao makundi yanawaharibu wanaishi maisha ya kuiga na kutamani vitu nje
ya uwezo wao.
Ushauri wangu adui wa mwanamke ni yeye
mwenyewe na pia kutokana na mfumo uliopo
tangu awali wanawake ni viumbe hafifu na
wengi wanafahamu hivyo na hawataki kuchukua hatua, wainuke na waseme hapana
inapobidi kusema hapana. Wanaume nao nawaomba waache kuwakatisha tamaa wake
zao bali wawatie moyo kwani wanawake
wakitiwa moyo na nguvu wana ujasiri kuliko hata wanaume, pia kuna wakati wawasaidie majukumu ya nyumbani kama yanakuwa mengi. Pia wanawake ni wazuri katika kutunza fedha. Nawaomba wanawake wenzangu wajidhatiti katika
kusimamia kile walichonacho ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea ya
maendeleo.
Wezesha na wadau wengine
hatutaacha kuwatia moyo wakati wote watakapohitaji ushauri wa kitaalamu. Kauli Mbiu yetu siku zote: “Wakiwezeshwa wanaweza”
Karibuni
tulishirikiane kulijenga Taifa letu kwa bidii na maarifa.
Lusako
Mwakiluma
Mhamasishaji
na muinuaji waliokata tamaa
Tuesday, December 27, 2016
WEZESHA TRUST FUND - MOROGORO YAFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA
WEZESHA TRUST FUND WALIPOTEMBELEA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA CHA BIGWA - MGOLOLE
TAREHE 26/12/2016.
WALITOA MISAADA MBALIMBALI KUSHEREHEKEA SIKU YA KUFUNGUA ZAWADI
PAMOJA NA WATOTO HAO
WALITOA MISAADA YA SAMAKI, NYAMA, MATUNDA, SABUNI, SUKARI NA VINYWAJI MBALIMBALI
Wafanyakazi wa Wezesha Trust Fund - Morogoro wakisaini kitabu cha Wageni Bigwa Mgolole - Kituo cha kulelea watoto yatima kutoka kushoto Mkurugenzi Bi Lusako Mwakiluma, Daktari Dr Elias Yuda Mtungilwa, Msaidizi wa Utawala na Mwalimu wa Tehama Maines Richard, Afisa Mafunzo Mohamed Nyongo.
Wezesha Trust Fund wakifurahi pamoja na Sista mlezi pamojawatoto yatima mara baada ya kukabidhi misaada, watoto walifurahi sana kupokea zawadi zao.
Wafanyakazi wa Wezesha Trust Fund wakiwabembeleza watoto yatima ambao ni wachanga wanaolelewa katika kituo hicho,
Wezesha Trust Fund kwa pamoja inaiomba jamii kuwa na tabia ya kuangalia watoto kama hawa katika vituo vilivyo karibu na mbali kwani ni faraja kubwa kuhakikisha yatima wanapata furaha kama watoto wengine. Yatima ni watoto wetu tusiwatenge wala kuwabagua.
Wezesha Trust Fund wakiwa pamoja na watoto yatima wa darasa la kwanza na pili - kituoni hapo wakiongozwa na Derick na David(mapacha) ambao tangu wakiwa na siku tatu baada ya kuzaliwa na kufiwa na mama yao Wezesha inawatembelea na kila wanapowaona wafanyakazi wa Wezesha wanafurahi sana.
Mungu wabariki walezi wa watoto hawa yaani Masista wote wanaohusika na pia wabariki watoto yatima wote wakue katika maadili mema na kumtegemea Mungu.
Sunday, December 25, 2016
USIMKOPESHE RAFIKI AU NDUGU YAKO
Kwa nini
leo nimefikiria haya? Naomba nikwambie
pesa ni jawabu la mambo yote namadhambi yote yameanzia kwenye pesa. Unaweza kuwa na rafiki au ndugu mliyeshibana
sana lakini pesa ikaja kuwatenganisha kwa urahisi mno na mkachukiana
milele. Pesa inatengeza marafiki na pia
inaleta uadui ndani yake. Basi ili uishi
kwa amani kila kitu unatakiwa ukifanye kwa kiasi.
Kila
wakati fanya msaada wa kipesa kama zawadi usifanye kama mkopo. Kama haujampa mtu msaada wa kipesa urafiki wenu unaenda kuisha
taratibu. Kama uko kwenye eneo la kuweza kumsaidia mtu basi msaidie usimkopeshe
mpe tu. Na kama unajua hauwezi kumpa
usimkopeshe itaenda kukuumiza wewe mwenyewe
(Ron Henley).
Sababu
ya kutompatia mkopo rafiki au ndugu wa karibu ni kwasababu ya kuondoa usumbufu
usio wa lazima wa kudaiana pasipo mashiko. Uhusiano wenu unaenda kuvunjika kama
sio kuharibika kabisa. Sababu ya watu
inayowapelekea kupata matatizo ya kipesa ni kutojua jinsi ya kufanya kazi na pesa
au jinsi ya kutumia fedha. Ukiwakopesha
wala hawajui wanaenda kufanyia nini kwani hawajajiandaa cha kwenda kufanyia
hizo pesa.
Kabla
ya kufahamu hivyo watachukua pesa kwako tena wataanza kutoa udhuru wa kushindwa
kukurudishia. Kinachofuata hapo ni
kukukimbia kila wanapokuona. Kuacha
kupokea simu yako na mwisho kutofungua mlango mara unapopiga hodi majumbani
kwao.
Naomba
kwa ushauri kama unataka kumsaidia ndugu yako au rafiki mpatie pesa kama msaada
na sio mkopo ili uishi kwa amani kwani utakapomkopesha hiyo pesa usiihesabu
katika akiba yako kwani imeondoka na hauwezi fahamu itarudi lini.
Hii ni
kwa faida yako ya watu wengine.
Karibu tusaidiane
pale tuliposhindwa na tunapoweza tuelekezane.
Kwani
maarifa ni mali kuliko pesa.
Lusako
Mwakiluma
Mhamasishaji
na Muinuaji kwa waliokata tamaa na kuugua
27 Desemba,
2016
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)