BREAKING NEWS

VIDEO

BIASHARA

USHAURI WETU

Friday, September 9, 2016

MECHI KATI YA POLISI MORO NA MAWENZI MARKET SIKU YA WEZESHA DAY AGOSTI-2016

Bonanza lililofanyika siku ya “WEZESHA DAY” ni Mechi kati ya Mawenzi Market na Polisi Moro lilidhaminiwa na Wezesha Trust Fund ili kuchangia kufanya utafiti na kukuza vipaji kwa vijana wetu kwenye Muziki wa kuimba na kucheza.  Mgeni Rasmi wa Shughuli nzima alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi – Wezesha Trust Fund Mheshimiwa Odilo Tweve.

Mheshimiwa Odilo Tweve alisema; nanukuu ndugu wanajamii nawaambia michezo ni afya, michezo ajira, michezo pesa na michezo ushirikiano na mshikamano katika jamii, tunakutana, tunabadilishana mawazo pia tunafurahi pamoja.  Hivyo basi tuendeleze vipaji vya vijana wetu ili tuweze kuwanusuru vijana waishio katika mazingira hatarishi, kwani watoto wa mazingira hatarishi tunawapenda na ni watoto wetu, tuwakimbilie, tuwahoji na tuwasaidie ili kujenga Taifa la Tanzania.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wezesha Mheshimiwa Odilo Tweve, akitambulishwa wachezaji wa Polisi Moro na Mawenzi Market kabla ya Mechi kuanza.
Mwenyekiti wa Bodi Mheshimiwa Odilo Tweve akiwaasa  wachezaji kabla ya Mechi kuanza kati ya Polisi Moro na Mawenzi Market  siku ya Wezesha Day


Wachezaji wakisikiliza kwa  makini ushauri nasaha kutoka kwa Viongozi wa Wezesha Trust Fund - Morogoro kwani michezo ni afya, michezo ajira na michezo ni ushirikiano na mshikamano.

  SHUKRANI KWA JAMII

Tunapenda pia kuwashukuru wote waliotuunga mkono kwa hali na mali ili kufanikisha shughuli nzima kwani tumemuona Mungu kwa namna ya tofauti na na tunaihakikishia jamii kwamba lazima watoto waishio mazingira hatarishi wapate muafaka wa matatizo yao kama sio kwisha kabisa. Kwani tulichopata si haba kuweza kufanikisha  malengo ya watoto na vijana hawa.

KAULI MBIU YA WEZESHA DAY:

“Watoto waishio mazingira hatarishi tunawapenda”


Lusako Mwakiluma
Mkurugenzi
Wezesha Trust Fund

Kwa niaba ya Bodi ya Wezesha na Wafanyakazi wote.

Umoja ni Nguvu, Utengano ni dhaifu

“HAPA KAZI TU”

Post a Comment

 
Copyright © 2013 WEZESHA TRUST FUND
Powered by WordPress24x7