BREAKING NEWS

VIDEO

BIASHARA

USHAURI WETU

Friday, September 9, 2016

WEZESHA TRUST FUND KUTIMIZA MIAKA MINNE KWA USAFI NA BONANZA - MOROGORO


Wezesha Trust Fund imetimiza miaka minne tangu kuanzishwa Agosti, 2016  kwa kuwa karibu na Jamii inayoizunguka kama vile Hospitali ya Sabasaba iliyoko katika kata ya Mafiga na Uwanja wa Taifa, nia na madhumuni ni kuonyesha mfano kwa jamii  kwamba tunatakiwa tufanye usafi katika maeneo yetu bila shuruti tukiamini usafi unaanzia nyumbani.  

Wezesha ofisi zake ziko Kata ya Uwanja wa Taifa, pia Wezesha ni Asasi ya kijamii ambayo inafanya kazi pamoja na wanajamii  na kupitia kazi hizo kunaifanya Wezesha kujua matatizo ya jamii inayoizunguka na kuweza kuyatatua yale yaliyo ndani ya uwezo na yale yaliyo nje kuyapeleka kwa Serikali - Kiwilaya na Kimkoa ili kuweza kuyapatia ufumbuzi wa kina.

Pia iliandaa Bonanza kubwa la Mpira wa Miguu na kuinua vipaji kwa vijana katika muziki, kuimba na kucheza ili kuweza kuwapeleka mbele zaidi.  Mechi kati ya Mawenzi Market na Polisi Moro ilichezwa na makusanyo ya kiingilio kilichopatikana yalienda kusaidia  kufanya utafiti kwa waishio katika mazingira magumu  wanaofanya shughuli zao Mawenzi Sokoni na nyingine zitawaandalia stadi za kazi baadhi ya watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane(18) na wale wakurudi shuleni chini ya umri wa miaka (18) watarudishwa kwa mujibu wa sheria.


Wafanyakazi wa Wezesha Trust Fund wakifanya usafi katika Hospitali ya Saba-Saba Mkoani Morogoro katika kuadhimisha siku ya WEZESHA DAY - AGOSTI, 2016.  Tukianzia na kushoto ni Mkurugenzi Bi Lusako Mwakiluma, Abubakari Mkingiye, Mohamedi Nyongo, John Ndumbalo, Wellingtone Maselle na Salum Tindwa. 

Tunakwenda sambamba na  Kauli mbiu ya Rais wetu Mheshimiwa Dr John Pombe Magufuli.  
Hapa Kazi tu!!!


Lusako Mwakiluma
Mkurugenzi
Wezesha Trust Fund

Kauli Mbiu - "Wakiwezeshwa wanaweza"

Post a Comment

 
Copyright © 2013 WEZESHA TRUST FUND
Powered by WordPress24x7