BREAKING NEWS

VIDEO

BIASHARA

  • JINSI YA KUMJALI MTEJA KATIKA BIASHARA YOYOTE

  • USHAURI WETU

    Tuesday, October 4, 2016

    KILA NYUMA YA MWANAMKE JASIRI YUKO YEYE MWENYEWE



    Kama watu wana wasiwasi kwa ukubwa wa mafanikio uliyonayo,  wewe endelea kufanikiwa zaidi  hautawasikia tena wakisema kuhusu wewe.

    Maisha ya mwanamke shujaa/Jasiri yana ushuhuda mkubwa sana, ukimkuta mwanamke amefanikiwa basi ujue kuna kitu amepitia pamoja na machozi yake atajifuta kisha atasema nina nguvu, sio kila unamuona kafanikiwa unataka uwe kama yeye, kama inawezekana muulize safari yake atakuambia ni safari ndefu yenye milima na mabonde lakini mwisho wake atakwambia niko peke yangu pamoja na yote haya. “nyuma ya mwanamke jasiri yuko peke yake”. 

    Huwezi kuwa jasiri kama mwanamke halafu ukawa na mtu nyuma yako ni wewe tu, kwani wanawake wengi hawataki mafanikio kama yako ila wanataka habari zako na kukutangaza kwa mabaya yako.  Naomba mwambie Mungu muweza wa yote kwamba ili nalo litapita.  Kwani hakuna jambo lisilo na mwisho katika maisha ya mwanadamu yeyote awe mzungu, burushi au budha, Muhindi hata Mbantu.  Endelea kumuomba Mungu siku zote,  muomba Mungu hachoki.

    Mpendwa wangu, mwanamke mwenzangu naomba nikuhakikishie simama katika nafasi yako, fanya kazi kwa bidii jiamini peke yako, watu ni wengi lakini binadamu ni wachache.  Acha tufanye kazi kwa faida yetu wenyewe na familia zetu.  Kwani mtafutaji hachoki na hakichoka amepata, hata Bakhresa ana pesa lakini bado anatafuta usiku na mchana.  Mtangulize Mungu katika kila jambo lako.  Naye atakupa unachokitaka kwa wakati wake.


    Lusako Mwakiluma
    Motivational & Inspirational Speaker
    Wezesha Trust Fund - Tanzania


    Post a Comment

     
    Copyright © 2013 WEZESHA TRUST FUND
    Powered by WordPress24x7