Kama watu wana wasiwasi kwa ukubwa wa
mafanikio uliyonayo, wewe endelea
kufanikiwa zaidi hautawasikia tena
wakisema kuhusu wewe.
Maisha ya mwanamke shujaa/Jasiri yana ushuhuda mkubwa
sana, ukimkuta mwanamke amefanikiwa basi ujue kuna kitu amepitia pamoja na
machozi yake atajifuta kisha atasema nina nguvu, sio kila unamuona kafanikiwa
unataka uwe kama yeye, kama inawezekana muulize safari yake atakuambia ni safari
ndefu yenye milima na mabonde lakini mwisho wake atakwambia niko peke yangu
pamoja na yote haya. “nyuma ya mwanamke jasiri yuko peke yake”.
Huwezi kuwa jasiri kama mwanamke halafu ukawa
na mtu nyuma yako ni wewe tu, kwani wanawake wengi hawataki mafanikio kama yako
ila wanataka habari zako na kukutangaza kwa mabaya yako. Naomba mwambie Mungu muweza wa yote kwamba
ili nalo litapita. Kwani hakuna jambo
lisilo na mwisho katika maisha ya mwanadamu yeyote awe mzungu, burushi au budha,
Muhindi hata Mbantu. Endelea kumuomba
Mungu siku zote, muomba Mungu hachoki.
Mpendwa wangu, mwanamke mwenzangu naomba
nikuhakikishie simama katika nafasi yako, fanya kazi kwa bidii jiamini peke
yako, watu ni wengi lakini binadamu ni wachache. Acha tufanye kazi kwa faida yetu wenyewe na
familia zetu. Kwani mtafutaji hachoki na
hakichoka amepata, hata Bakhresa ana pesa lakini bado anatafuta usiku na
mchana. Mtangulize Mungu katika kila
jambo lako. Naye atakupa unachokitaka
kwa wakati wake.
Lusako Mwakiluma
Motivational & Inspirational Speaker
Wezesha Trust Fund - Tanzania