MBINU 6 ZITAKUSAIDIA SANA
Kutokana na mabadiliko ya
tabia nchi na hali ya kukua kwa uchumi mambo mengi yamebadilika sana, Hivyo
basi ni muhimu tujifunze njia za kujiimarisha ili tuweze kupita salama katika
hali hii, usipoteze muda kulalamika amka anza kuangalia mbinu hizi ili uboreshe
maisha yako. Nenda na dira usiwe
mchelewaji wah sana uone faida ya kuwa wa kwanza katika kutatua matatizo na
kupata fursa zilizopo karibu uone mbinu ambazo zitakusaidia kuinuka kiuchumi
kwa haraka.
1. Uhuru wa fikra: Kama kuna nyakati ambapo
unahitaji uwezo wa kuiona dunia kama ilivyo na sio kama unavyotaka iwe, basi ni
sasa. Ni muhimu kuboresha ufahamu wako wa mambo mengi ya kimsingi ya kimaisha
kama vile mapenzi, biashara, tabia, teknolojia ,, na zaidi sana maswala ya kiroho.
Uhuru wa kifikra
utakuwezesha uweze kujitawala vema, kwani kimsingi wewe ndiye mtu wa kwanza
kabisa unayeweza kuleta mabadiliko makubwa na maendeleo kwa maisha yako,
kwakuwa unayo nguvu ya utashi, kufanya
maamuzi au kuacha watu waamue mambo kwa ajili yako.
2. Kuboresha mtandao: Kwakuwa unahitaji kutambua fursa
nyingi kwa kadri inavyowezekana na kwa kuwa wewe ni mzalishaji, unahitaji sana
kujenga mtandao mkubwa na mtandao wenye manufaa ili kuweza kutambua fursa
mbalimbali kupitia mtandao wako, na pia kuweza kuuza bidhaa zako kupitia
mtandao huo.
3. Kuwa mzalishaji: Katika machafuko
haya, bidhaa na huduma mbalimbali zitakuwa adimu, na kwa
wazalishaji wachache watakaoweza kuzalisha kwa ufanisi wataweza kujikuta
wakiendesha maisha vizuri. Hivyo pamoja na kuwa
mtumiaji wa fedha zako kwa mambo ya burudani, unahitaji kuhifadhi fedha zako
kwa namna ambayo fedha zako hazitopoteza thamani zake, na wakati huo huo,
ukifanya utafiti wa aina ya bidhaa au huduma ambazo utakuwa ukizalisha, ili
nawe unufaike na mazingira tuliyonayo. Kuendelea kuwa
muingizaji wa kipato (kwa njia ya ajira pekee) na kuwa mtumiaji zaidi ya
mwekaji akiba, si jambo la busara, hasa katika hali ngumu ya kiuchumi na
kijamii tuliyonayo.
4. Kuwa mwepesi wa kubadilika: Mambo mengi yanabadilika
kwa haraka sana, ufahamu uliokuwa nao jana , mbinu ulizotumia siku za nyuma hata kama zilifanikiwa, inawezekana kabisa
zisifanikiwe kwa sasa, na kwa kadri mambo yanavyozidi kubadilika. Ushindi wa
kipekee unakuja pale unapoweza kuwa mwepesi wa kubadilika, kwa kubuni njia mpya
na bora za kukabiliana na mazingira unayokumbana nayo.
5. Kaa tayari kwa kusafiri: Fursa zinaweza kutokea popote pale, hivyo kuwa tayari
kusafiri nje ya mkoa uliopo sasa, na zaidi sana nje ya nchi. Hakikisha una
passport halali na isiyoisha muda wake, na tambua taratibu za kusafiri nje ya
nchi, kama vile mambo ya visa, na gharama
za maisha kwa nchi tofauti.
6. Mipango ya muda mrefu: Tambua kuwa hali
hii ngumu ya maisha ni swala ambalo litaendelea kwa muda mrefu, hivyo ni muhimu
kujipanga wewe na familia yako. Kama una watoto au una mpango wa kuwa na
watoto, basi ni wakati wa kufikiria pia namna ya kuja kuwawezesha watoto wako
wawe na ujuzi wa uhakika, na kuwa wawe wazalishaji. Hakikisha unajitengenezea ujuzi na uzoefu uliokomaa
katika jambo fulani au mambo kadhaa tofauti, ili uweze kuja kuuza ujuzi na
uzoefu wako huo katika soko gumu la huduma tunalokumbana nalo kwa nyakati za
leo na zijazo.
Lusako Mwakiluma
Muhamasishaji na Muinuaji
January, 2017
Post a Comment