Hii
ni hali ya kisaikolojia. Angalia
kupata zaidi kutoka na neno linalokwenda.
Uangalie mitihani kama mtu anayekuja kukudai deni lako na
anataka wewe umlipe. Hapo utaongozwa na hali ya wakati huo. Wewe ni
mdeni unayedaiwa. Wewe ni mhusika. Kuwa mhusika mkuu au mdaiwa
inakupa ujasiri. Kuwa jasiri
Kuwa jasiri maana yake
unatakiwa kukabili hali hii bila hofu.
Mfano; Unatakiwa sasa ulipe deni
na mdeni nae hataki kuondoka mpaka umpe
pesa yake, kama ni wewe unafanyaje? Unatakiwa uwe mtulivu kisha umpe mikakati
ya jinsi ya kulilipa deni aidha umechelewa
kuna sababu itabidi umpe za kumfanya aridhike na kuweza kukuongezea muda
wa kuweza kulipa kama ulivyomuahidi.
Usimkimbie wala usikatae kuongea naye
utapoteza ujasiri wa kukabiliana na mitihani yako.
Muhammad Ali, alikuwa bingwa wa mchezo wa
saikolojia. Aliingiza hofu ndani ya moyo
wake kabla ya kupigana kwa njia ya kutengeneza ushindi kabla ya pambano. Ali alikuwa
anatafakari ushindi wakati
wote. Alikuwa anapigana
kisaikolojia na mwishoni aliingia
ndani ya uwanja kama mshindi siku ya pambano kwani aliweza kumsoma anayepambana
naye kupitia michezo ya nyuma.
Wengi wameshindwa kumpiga Muhammad Ali na walikuwa wanapigwa
kabla hata mchezo haujaanza.
Geogre Foreman alikuwa na uzito mkubwa
katika siku zake za mapigano. Watu
wachache waliweza kupigwa kwenye mzunguko wa
kwanza tu walipopigana nae.
Foreman alikuwa na uzito mkubwa sana kuliko mahasimu wake. Kabla ya mchezo ambao sitausahau na George Foreman
kule Zaire. Ali alizungumza na dunia jinsi alivyojiandaa kupigana na huyo
hasimu wake. Alijihakikishia ushindi na
alikubali yote kwamba anaenda kufanya
kitu cha tofauti.
Ndiyo, unaweza kufikiria kitu gani
kilitokea siku hiyo ya mpambano. Kwa wakati
ule kengele ilipopigwa kwa mara
ya kwanza, George Foreman alikuwa ni mtu aliyepigwa tayari. Ali alijitahidi kumtoa nje kwa mazungoko wa
kwanza tu.
Jiandae na wewe kwa mtihani kama Ali
alivyojiandaa kupigana na George
Foreman na hakuwa na hofu ya kupigana
naye (Work Hard, Work Smart then Trust God).
Nawasilisha.
Lusako Mwakiluma
Post a Comment