MTEJA ndiye mtu muhimu sana katika biashara yako. Hakuhitaji wewe ili
kuishi, bali biashara yako inamuhitaji ili iendelee kudumu na wewe uweze
kuishi. Kumbuka mteja wako asiporidhika, atakwenda sehemu nyingine
atakaporidhishwa.
Kila wakati fahamu kwamba, mteja wako ni mtu muhimu sana ama awe amekuja
yeye mwenyewe moja kwa moja kwenye biashara yetu au awe ametupigia simu au
kutuandikia, tunapaswa kumjali na kumhudumia vizuri kama ipasavyo bila kuwa na
visingizio!
Mteja
hatuletei bughudha kwenye biashara yetu…yeye ndiye kusudi kuu la biashara yetu.
Anatupatia upendeleo wa kipekee kwa kutupa sisi nafasi ya kumhudumia.
Mteja
siyo mtu wa kubishana naye au kujaribu kushindana naye kwa maneno ili
kumuonesha sisi ni wajuaji kiasi gani. Hakuna aliyewahi kushinda mabishano na
mteja wake. Kwa namna yoyote mabishano makali yanaathiri biashara yako.
Tumia hekima na diplomasia kadiri iwezekanavyo.
Mteja
ni mtu anayekuja kwetu kwa kuwa anahitaji huduma au bidhaa fulani hivyo ni kazi
yetu kumtimizia mahitaji yake kwa njia ambayo ni ya faida kwetu na kwake pia.
Mteja
siyo namba tu au takwimu, bali ni binadamu kama vile mimi na wewe. Ana hisia
kama zile tulizonazo; hasira, furaha, njaa, kiu, uchovu, msongo wa mawazo, n.k.
Kutokana
na haya machache niliyosema hapo juu, mteja ni mtu muhimu sana kwa biashara
yetu, bila yeye biashara haiwezi kuwepo! Hivyo kama hujui namna ya kuwa mtaalam
wa biashara yako, basi anza na sehemu hii muhimu ya biashara yako, halafu
utapanua ufahamu wako kwa sehemu zingine.
Au
kama umewaajiri wengine kwa ajili ya kushughulika moja kwa moja na wateja, basi
hakikisha kuwa unawapatia maarifa haya kwa kupitia wataalam wa biashara, semina
za ujasiriamali au wewe mwenyewe kuwafundisha, kuwahamasisha au hata
kuwakumbusha kila wanaposahau.
Ni
muhimu kufahamu kwamba watu wengi wanashindwa kila siku katika ulimwengu wa
biashara kwa kuwa tu hawana maarifa katika vipengele mbalimbali vya biashara.
Eneo jingine ambalo ni lazima uwe mtaalam bila kushindwa hata kidogo ni eneo la
uuzaji. Ninaposema uuzaji nina maanisha uwezo wa kuwashiwishi wengine waweze
kununua bidhaa yako, kukubali wazo lako au kujiunga na biashara yako.
Zamani nilipoanza kujifunza
mbinu za kuwa tajiri kwenye ujasiriamali nilikutana na kanuni ifuatayo ambayo
ni rahisi sana kuilewa:
Mauzo = Kipato.
Kwa lugha nyingine wewe kama mfanya biashara unapaswa kujiuliza mara kwa mara maswali kama yafuatayo:
“Nitawezaje kuongeza mauzo ya biashara yangu?”
Mauzo = Kipato.
Kwa lugha nyingine wewe kama mfanya biashara unapaswa kujiuliza mara kwa mara maswali kama yafuatayo:
“Nitawezaje kuongeza mauzo ya biashara yangu?”
“Nitawezaje kufanya hawa
wateja nilionao waniletee wateja wengine zaidi?”
“Ni wapi ambako ninaweza kupata wateja wenye uwezo wakununua kwa wingi zaidi kutoka kwangu na kwa idadi kubwa kadiri iwezekanavyo?”
“Ni wapi ambako ninaweza kupata wateja wenye uwezo wakununua kwa wingi zaidi kutoka kwangu na kwa idadi kubwa kadiri iwezekanavyo?”
“Nitumie mbinu gani ili wateja
wanapokuja kwenye eneo langu la biashara waweze kununua zaidi ya wanavyonununua
sasa?”
Maswali kama haya mpendwa msikilizaji yana uwezo wa kubadilisha mapato kwenye biashara yako kuliko namna nyingine yoyote ninayoifahamu. Hivyo tenga muda kila siku japo kwa nusu saa au saa moja, kuwa peke yako na jiulize maswali magumu kama haya, kisha andika majibu kwenye kila kidaftari kidogo kila unapopata wazo jipya.
Kimsingi hii ndiyo siri kuu ya
ushindi ya bilionea Richard Branson mwenye makampuni yenye nembo ya Virgin
yanakadiriwa kuwa zaidi ya mia tatu ulimwenguni kote.
Mwingine ambaye siri hii ilimtoa ni ndugu Sam Walton ambaye ndiye mwasisi wa supamaketi za Wal-mart zilizozagaa ukimwenguni kote. Inasemekana kwamba wakati ndugu Walton anaanza biashara yake miaka mingi iliyopita kama mmiliki wa duka dogo tu lililouza vitu vya nyumbani alikuwa na tabia ya kwenda kujifunza.
Mwingine ambaye siri hii ilimtoa ni ndugu Sam Walton ambaye ndiye mwasisi wa supamaketi za Wal-mart zilizozagaa ukimwenguni kote. Inasemekana kwamba wakati ndugu Walton anaanza biashara yake miaka mingi iliyopita kama mmiliki wa duka dogo tu lililouza vitu vya nyumbani alikuwa na tabia ya kwenda kujifunza.
Hivyo alijifunza walivyopanga
bidhaa zao, walivyopunguza bei , walivyokuwa wakiongea na wateja n.k,
Inasemekana kwamba Sam alikuwa ana tabia ya kuwahi kwenye supamaketi hizo
asubuhi sana kabla hawajafungua na kupaki pick up yake nje na kusubiri
wafungue.
Na mara tu walipofungua
aliingia ndani na kidaftari chake kidogo na kuandika kila kitu alichojifunza
ndani ya lile duka, aliporudi kwenye duka lake alijaribu kuiga mambo mengi kama
alivyojifunza. Kwa lugha nyingine alikuwa ana copy na ku-paste! Lakini
yeye hakuishia hapo tu bali alikuwa ana-copy, halafu ana-improve na ku-paste.
Leo hii japo Sam hayuko pamoja nasi amewaachia watoto wake utajiri mkubwa, wana maduka zaidi ya 8000 dunia nzima na wana mamilioni ya wafanyakazi ulimwenguni kote.
Post a Comment