Kama binadamu
unatakiwa ujitambue ili uweze kwenda na
wakati au kufanya yale ambayo yanatakiwa
kufanyika na yale ambayo
hayatakiwi kufanyika usiyafanye.
Kuna
mambo ya msingi ya kuyafanya ili uweze kufikiria vizuri
wakati wote. Na kila mtu
atakayekuona atajua huyu mtu amejitambua
na amejua umuhimu wake katika jamii
inayomzunguka kwani utajikubali wakati
wote na kuwaheshimu wengine.
Moja
Fikiri vizuri
(jenga mfumo wa kufikiri vizuri); mfumo huu uwe endelevu; siyo usubiri upate
tatizo ndiyo uanze kufikiri vizuri (usiwe kama zima moto). Hii itakusaidia kuanza kupanda mbegu njema kwenye mawazo yako
ya kina ili maisha yako ya baadaye yawe
mazuri; yatoe mbegu nzuri/njema.
Mbili
Rudisha
mawazo yako nyuma, jenga picha yako ya
utotoni. Chagua taswira moja wakati
ulipokuwa mtoto jione kimwili, kimavazi na mazingira ulipokuwa (nyumbani
/shuleni au popote). Kisha rudi kwako
sasa hivi ukiwa mtu mzima; jione kama ulivyo sasa hivi ukiwa unamtazama huyo
mtoto ambaye umemjengea taswira; mtoto ambaye
pia ni wewe. Mtazame na zungumza
naye, mwambie ulidanganywa kwamba ni mbaya; huna akili, huna thamani,
huwezi, hufai nk; na wewe uliamini kwa
sababu ulikuwa mtoto. Lakini sasa umekuwa
mkubwa; fahamu ukweli halisi kwamba wewe ni mzuri, una akili unaweza na una
thamani sawa na wengine; unaweza na
unafaa. Rudia zoezi hili mara kwa mara;
kila wakati hakikisha unachagua eneo ambalo
uliambiwa huwezi; Futa imani zote mbaya kwenye mawazo yako ya kina.
Tatu
Ni ile ya
kufanya zoezi la kurudia rudia maneno pamoja na kujenga taswira mfano: kila wakati jiambie ninaweza; ninafaa; nina thamani,
najiamini. Imani ni muhimu sana wakati
unajimbia maneno hayo.
Nne
Hapa utaenda
kutumia mshumaa, uwashe mshumaa; uweke mbele yako juu ya meza au stuli au
sehemu yoyote. Angalia ile sehemu ya mshumaa inayowaka moto (siyo mshumaa wote)
kwa muda wa dakika 10, 30 au zaidi.
Baada ya hapo fumba macho yako yote ili uuone ule moto wa mshumaa kwa kutumia macho yako ya akili (yaani jicho
la tatu). Utaenda kuona moto huo ukiwa
wa kijani, bluu, njano au mweupe. Baada
ya kuuona, anza kuchoma zile tabia au
mambo yanayokukera au kuwakera wengine mfano: Choyo, wivu, uzinzi, dharau,
zichome moja baada ya nyingine. Wakati unazichoma utaona moto wa mshumaa
ukiongezeka ukubwa au utaona moshi. Fanya zoezi hili mara kwa mara. Baada ya muda
utashangaa kuona tabia au mambo hayo yamekwisha na tabia hizo umeziacha kabisa.
Tano
Ni ile hali
ya kutumia kioo, simama jitazame kwenye kioo ikiwezekana kila siku asubuhi na
jioni. Tafuta zile kasoro ambazo
uliambiwa na jiambie kwamba huna. Kama uliambiwa wewe ni mbaya; Basi jiambie
wewe ni mzuri, huku ukijiangalia bila kujiogopa kwenye kioo. Lakini kama uliambiwa huwezi, jiambie naweza
sana. Pia jikubaai kama ulivyo na
jiambie umekamilika, una thamani na unastahili.
Sita
Ni ile hali
ya kupata nafasi ya kuyapa mawazo yako ya kawaida baada ya kupewa nafasi ya muda hatimaye yatachukuliwa mawazo yako ya kina,
mambo haya mapya yataua au kukausha ile miche/miti
iliyoota kwenye mawazo yako ya kina; miti hii ni ile ya mambo ambayo
yanakukera au kuwakera wengine. Kwa ile ambayo imeshazaa matunda haiwezi
kukauka kwani umeshaanza kuvuna kitu ambacho nidyo maisha unayoishi hivi
sasa. Njia hizo zote tano ni za
mzunguko. Hii ya sita ni ya njia ya mkato kwani unaenda moja kwa
moja kwenye mawazo yako ya kina na
kuyaambia yale unayoyahitaji ambayo ni kinyume na yanayokukera.
Nguvu
ya uumbaji kitaswira na kujipa nguvu
(i)
Kumbuka: Imani – hisia-
matokeo
(ii)
Ondoa mipango ya zamani
kwenye mawazo ya kina ndiyo sababu ya
msingi ya kukwama kwani nyuma ni historia na inatia uchungu ukiifikiria.
Kuna aina tatu ya uumbaji kitaswira: sauti, kuona na hisia.
(iv)
Kila mmoja ana aina yenye
kutawala kwake awe anajua au la. Kuna
wengine wanatawaliwa na aina mbili. Katika matumizi ya uumbaji kitaswira,
tunaanza na aina yetu, baadaye tunajifunza nyingine.
(v)
Ili kujua aina yako, jaribu
kufikiria unachohitaji sasa hivi ili uone.
Mwanzoni unaweza kusikia sauti
inayokuambia hutaweza au ni mzaha ufanyao.
Unatakiwa ufanye mazoezi mengi ili uweze kujenga uwezo wako ulionao au
uliopotea.
(vi)
Mawazo
yako ndiyo yenye
kukufanya/kukuwezesha ujenge uumbaji kitaswira. Unachokiona kila siku
ni matokeo ya kilicho mawazoni kila siku. Hivyo, bila kujua huwa
tunaumba yale
tusiyoyataka maishani. Uumbaji kitaswira unawakilisha utunzaji wa
mbegu
(mawazo) kutegemea ni mbegu gani
tumepanda.
(vii)
Makosa
yajitokeza sana; usiweke nguvu
kwenye kukosa, kwenye usichotaka na kwenye usichonacho. Mfano: kama
umepanga kwenye chumba kimoja na unataka kujenga nyumba yako,
usijiambie nimechoka kukaa kwenye haka kakibanda au maisha ya kupanga
yamenichosha. Sema lazima niambie
nyumbani kwangu yaani nyumba niliyojenga mwenyewe.
(viii)
Unapokuwa kwenye uumbaji kitaswira, hisi au ona kama vile jambo limeshakuwa tayari – piga picha ya utayari wa jambo lako.
(ix) Jinsi ya kufanya (hatua);
(i)
Tafuta mahali tulivu
(ii)
Tuliza mawazo yako
(iii)
Weka nguvu zako za mawazo
katika jambo unalolitaka
(x)
Simamia kufikiria vizuri
wakati wote utakaokuwanao na utashangaa kuona matokeo mazuri na kwa muda mfupi
sana.
Ubarki
ReplyDeletewe sana
Ubarikiwe na mungu
ReplyDelete