Napenda kutoa mada fupi na ya kutiana moyo wenyewe kwa wenyewe,
kwa mtazamo wa macho ya nyama maisha ni magumu sana, lakini katika mtazamo wa
kiroho maisha ni ya kawaida na hayataki mashindano, unashindana na nani? Na
unaishi kwa ajili ya nani? Fanya kile kitu kina manufaa kwako na familia
yako ili kesho uje uburudike. Kwani kuishi ni leo kesho ni matokeo
unaweza ufike au usifike, jiwekee akiba kama vile vile unaishi milele halafu
muofie Mungu kama vile unaondoka(kufa) leo.
Watu wengi
wamechukua muda mrefu kutafuta furaha wameikosa, furaha inaanzia ndani mwako
(happiness is inside job) usikae ukisubiri mtu kukupa furaha, utapata ya muda,
jiangalie unataka nini na unaweza kufanya nini katika maisha yako? Jitume
sana, fanya sana kazi ili uweze kula matunda mema ya nchi. Na kumbuka
tunaufukuza upepo inabidi tuweze kumshukuru huyu anayetupa pumzi ya bure kwa
neema na rehema zake, wengi wanalia, wengi wamekata tamaa, wengi wanataka
kujiua na wengine wamesusa hata kuanza tena kwa kuanguka. Mwenye haki wa
Mungu huwa anaanguka mara saba kisha anainuka tena.
"With God there is second
chance"
La hasha wakati ni
huu tuamke na tutende yale tuliyoyandika kwenye vitabu vyetu kama ni malengo ya
mwaka 2016 najua kuna wengine hawajaandika. Maandishi yanadumu milele,
mazungumzo ni muda mfupi tumia muda wako kuandika malengo yako na uyafanyie
kazi.
"see it, believe on it then you should
act on it and you shall see the results as soon as possible"
Hii ni changamoto
kwani kila siku angalia umefanya nini na ikifika jioni piga mahesabu ya masaa
uliyotumia kwa kufanya kitu hata kimoja cha maana.
Wako muuinuaji na
mtia watu moyo hata kwa yale yanayoonekana magumu, imani pasipo kuona.
Lusako Mwakiluma
Post a Comment