Watu wengi wanakufa masikini na wanashindwa kufikia mafanikio yao bila wao kujua tatizo ni nini,imekuwa kama ugonjwa watu wengi kuendelea kulalamikia serikali au wazazi wao kuwa wao hawafanikiwi wao ndio sababu,na wengine wamekuwa wakikata tamaa kabisa ya mafanikio yao bila wao kujua nini kinachokwamisha maisha yao kuwa bora.Leo tutajifunza pamoja vizuwizi vya mafanikio yako ambapo kama utavifanyia kazi basi utaanza kushuhudia mafanikio yako,ni muujiza mkubwa sana utatokea kwako hakuna aliezaliwa kuwa masikini rafiki.soma kwa makini.
1.UOGA(Fear)
Hichi ni kikwazo kikubwa sana kwa watu wengi ktk mafanikio yao,watu wengi wamekuwa masikin na wengine kufa masikin kwasababu ya uoga,uoga wa kukataliwa na uoga wa kushindwa,kama unataka kufanikiwa ktk kila kitu kwenye maisha yako usiogope kuomba au kusema chochote mbele ya watu eti kwa kuogopa kukataliwa rafiki usiusemee moyo wa mwenzio usiogope,lkn pia usiogope kushindwa yani mtu anataka kufanyabiashara lkn kitu cha kwanza anawaza ni kushindwa anaamini kuwa yeye hawezi na akianzisha atafeli.Rafiki acha uoga kwani huo ndio umasikin wako ushinde uoga ushinde maishani.USIOGOPE..
2. KUKOSA MSUKUMO (Lack of agressivenes)
Watu wengi wanashindwa kufanikiwa ktk maisha yao kwa sababu ya kukosa msukumo binafsi,ngoja nikwambie rafiki hakuna mtu yeyote ambae atakaa chini na kupanga maisha yako au kuna mtu ataacha shughuli zake kwaajili ya kupigania maisha yako,wewe ndio unaejua ugumu na uchungu wa maisha yako amka sasa kuwa na msukumo kutoka moyoni mwako wa kushinda maishani usisubiri fulani ndo akwambie nenda kazi,fanyabiashara wewe mwenyewe kaa chini jitume utafanikiwa.
3.UJASIRI NA KUJIAMIN (Courage and confidance)
Hpa ndipo balaa watanzania wengi hawajiamini rafiki hebu jiamini kuwa wewe unaweza ndani yako kuna mtu mkubwa saana,hebu acha kusikiliza watu wengine wanasema nini kuhusu wewe usikilize moyo wako unasema nini kuhusu wewe,usikubali kushindwa thubutu kwa kila jambo unaloambiwa lenye mafanikio na usiamini kuwa wewe huwezi unaweza rafiki.
4.KUKOSA LENGO MAALUMU (Lack of purpose driven goals)
Rafiki malengo yako nini? Lengo ni ndoto zenye mipaka,kuna malengo ya muda mfupi,muda mrefu na muda wa kati.wewe malengo yako ni yapi? rafiki hautakuja kufanikiwa ktk maisha yako kama huna malengo ya maisha yako kama huna malengo panga leo yaandike malengo yako.mtu asiye na malengo ni sawa na mtu ambae anaenda stendi kupanda gari lkn hajui anaenda wapi sasa atapanda gari gani na atashukia wapi huyu hata fika bali atazunguuka a ari hadi usiku gari linapokwenda kupaki basi litamshusha popote.JUA MALENGO YAKO RAFIKI UTAFANIKIWA.
5.KUTOKUJITOA (Lak of comittment)
Kujitoa limekuwa tatizo kwa watanzania wengi, ewe mtanzania jitoe kwaajili ya maisha yako acha uvivu wa kufikiria Mungu ashughuliki na wavivu jitoe pambana kwaajili ya maisha yako utafanikiwa.
6.KULINDA MUDA (Timemanagement)
Hahahahaaaa watu wengi wanaposikia mua ni mali huwa hawaamini leo nataka ujue kuwa muda wako ndio umasikini wako na ndio utajiri wako.unatumiaje muda wako ambao unatoka kazini? unatumiaje muda wako ambao unatocha chuo? wewe mama wa nyumbani unatumiaje muda wako ambao unakuwa hauna kazi nyumbani? hapa ndipo kasheshe na umasikini wa watu ulipo.iko kila sekunde na saa inayopita lazima uhakikishe unafanya kitu ambacho chenye manufaa kwenye maisha yako,mfano ukitumia masaa mawili unajifunza kitu chenye mafanikio kwenye maisha yako basi unayavuta mafanikio yako masaa mawili kama mafanikio yako yalikuwa uyafikie kwa siku mbili na masaa mawili basi utakuwa umebakisha siku mbili.kama unatumia muda wako kuangalia TV,kupiga umbea kupiga story zisizokuwa na maana ukifanya hivyo masaa mawili kwa siku ndani ya mwaka utakuwa umepoteza zaidi ya miezi 4,basi hiyo miezi minne ndio umesogeza mbele mafanikio yako.kwaiyo kama ungetakiwa ufanikiwe kwa miaka miwili basi utafanikiwa kwa miaka miwili na miezi minne.sasa watanzania wengi huwa wanapoteza zaidi ya miezi 9 kila mwaka ndani ya miaka 15 tayari ameshasogeza mbele mafanikio yao kwa zaidi ya miaka kumi.kwa hiyo ukichukuwa miaka kumi ya kutafuta maisha na ile miaka kumi aliopoteza ni miaka 20.ameanzakutafuta maisha na miaka 30-40 miaka ya kufikia mafanikio yake itakua 50 na maisha now ni mafupi hayafiki huko na kipindi anaendelea kutafuta anapoteza tena masaa kadhaa.lazima ufe masikini.amka sasa mtanzania acha kutumia muda wako vibaya kwani muda wako unaoupoteza sasa utakugharimu.
MUDA NI MALI UKIPUUZA HILO UTAKUFA MASIKINI.ACHA KULALAMIKA CHUKUA HATUA.
Karibu tutimize ndoto zetu pamoja.
SOURCE:BASSANGA CHANGING LIFE
Nimeamini chanzo cha umaskini ni sisi wenyewe tunapoteza malengo, muda na hata kujitoa ili tufikie malengo yetu. Tunakaa muda mwingi kwa kupiga soga na majungu yasiyojenga. Naamini kupitia mada hii ya mambo sita tutayafanyia kazi na kuweza kutimiza ndoto zetu.
ReplyDelete