BREAKING NEWS

VIDEO

BIASHARA

USHAURI WETU

Sunday, March 20, 2016

FIKIRIA KAMA MBUNIFU ILI UWE MTU MWENYE UMAKINI WAKATI WOTE

Wakati unafikiria mawazo yako ya ndani ni kwamba uko tayari kuzalisha kitu kizuri ulichobuni kama mbunifu;  Wakati wote unatakiwa kuwa hivyo ili uweze kuleta kitu cha tofauti katika jamii. Waangalie wabunifu wakubwa walioweza kutumia umakini na kuweza kubuni baadhi ya vitu ambavyo leo tunavitumia;-

Thomas Edison alifikiria akapata wazo kubadilisha ulimwengu wa Technolojia
Albert Eistein alifikiria akapata wazo la kubadilisha ulimwengu wa fizikia
Charles Darwin alifikiria akapata wazo la kubadilisha ulimwengu wa biolojia

Sio wote kwa upande wetu wanafanikiwa kwa kiasi cha kupata wazo zuri, tunaangalia kwa kufikiria ubunifu, mawazo mazuri na kupata suluhisho la jambo.

Kufika hapo unatakiwa uende kufikiria kila siku na uangalie ubunifu wako wa ndani kwa kutengeneza mawazo mengi na kuchukua kama tahadhari kama inawezekana.

Hapa angalia jinsi ya kutengeneza mawazo kama mbunifu:
Fikiria sana
Tengeneza mawazo mengi, mbadala na mwisho wake kama inawezekana usiwe na wasiwasi kuhusu  ubora wa wazo lako, ila ni mawazo mangapi unaweza kuwa nayo.  Kuna muda wa kuangalia tena baadaye na hata kama umemaliza kuyaangalia mawazo yote.  Kitu unachokitaka hapo ni kupata wazo moja tu kubwa.
Usijihukumu
Hata kama ukoje au upendi mawazo yako yaache yaje.  Kuangalia somo la nyuma kwa macho mapya, kama ulipitia kwenye hali hali ngumu jaribu kutazama kwa mtazamo mwingine mpaka upate wazo moja zuri. Hii itakusaidia kufikiria kitu katika ufahamu wako ambao huru, usijihukumu.
Tengeneza orodha
Andika chini au pengine tunza kwenye kumbukumbu kila wazo, hata kama unaona sio wazo zuri kwako.  Tena  wazo baya  unaliweka pamoja kwani ndani yako sio yote mawazo mazuri kama linakuja liweke tu unaweza ukalitumia mahala fulani na usijiweke katika sehemu ya kuchanganyikiwa kuhusu mawazo yako, subiri au  jiulize ni wazo langu mwenyewe? Baadaye unaweza ukaitumia hiyo orodha kupata faida kubwa.

 Changanua mawazo yako na uyaboreshe
Njoo na mtazamo wa wazo lako kwa kulipanga bila kufuatana au kutokuwa na umuhimu.  Angalia njia mbadala ya kufikiria kuhusu  somo hata kama  ni njia ya zamani lakini inafanya kazi.
Pika wazo lako na  na liiache liendelee mpaka lizalishe kitu
Panga muda  wa kupika  mawazo yako na yaruhusu  yaweze kuendelea kuzalisha mawazo mengine hii inachukua muda.  Fanyia kazi tatizo, tengeneza wazo, tena tembea  na fanya kitu kingine kabisa tofauti. Usifikirie kuhusu tatizo  wakati mwingine ila liache nyuma tatizo likiungua polepole. Unaweza ukashangaa ni wakati gani ndani kitu kinafanyika chenyewe, wakati wewe umeacha kiendelee chenyewe.

Wote tunataka kupata ubora mzuri na mawazo mazuri katika kila tunachokifanya.  Ili kuboresha njia nzuri ni kufikiria sana na jinsi tunavyojiongoza na jinsi tunavyoutunza muda wetu, hatua ya kwanza ni kuboresha  tunavyofikiria.  Je, unafahamu hivyo? Nakwambia utakuwa mtu mwenye umakini katika kila unachokifanya wakati mwingine popote ulipo.


Lusako Mwakiluma

Friday, March 11, 2016

MAISHA NI SAFARI YENYE MILIMA NA MABONDE

Wapendwa naamini kwa uwezo wa Mungu mmeshinda salama, leo napenda kutoa mada fupi na ya kutiana moyo wenyewe kwa wenyewe, kwa mtazamo wa macho ya nyama maisha ni magumu sana, lakini katika mtazamo wa kiroho maisha ni ya kawaida na hayataki mashindano, unashindana na nani? Na unaishi kwa ajili ya nani?  Fanya kile kitu ambacho kina manufaa kwako na familia yako ili kesho uje uburudike.  Kwani kuishi ni leo kesho ni matokeo unaweza ufike au usifike, jiwekee akiba kama vile unaishi milele halafu muofie Mungu kama vile unaondoka(kufa) leo.

Watu wengi wamechukua muda mrefu kutafuta furaha wameikosa, furaha inaanzia ndani mwako (happiness is inside job) usikae ukisubiri mtu kukupa furaha, utaipata furaha ya muda, jiangalie unataka nini na unaweza kufanya nini katika maisha yako?  Jitume sana, fanya kazi sana ili uweze kula matunda mema ya nchi.  Na kumbuka tunaufukuza upepo inabidi tuweze kumshukuru huyu anayetupa pumzi ya bure kwa neema na rehema zake, wengi wanalia, wengi wamekata tamaa, wengi wanataka kujiua na wengine wamesusa hata kuanza tena kwa kuanguka.  Mwenye haki wa Mungu huwa anaanguka mara saba kisha anainuka tena.  "With God there is second chance".

La hasha wakati ni huu tuamke na tutende yale tuliyoyandika kwenye vitabu vyetu kama ni malengo ya mwaka 2016 najua kuna wengine hawajaandika na hawana tabia ya kuandika malengo yao. Maandishi yanadumu milele, mazungumzo ni muda mfupi tumia muda wako kuandika malengo yako na uyafanyie kazi, "see it, believe on it, then you should act on it and you shall see the results as soon as possible"

Hii ni changamoto kwani kila siku angalia umefanya nini na ikifika jioni piga mahesabu ya masaa uliyotumia  kwa kufanya kitu hata kimoja cha maana "Do one good deed a day"

Wako muuinuaji na mtia watu moyo hata kwa yale yanayoonekana magumu, imani pasipo kuona itakupatia majibu ambayo ukufikiria.

Lusako Mwakiluma

Saturday, March 5, 2016

WANAWAKE NA FURSA-UJUMBE KWA WANAWAKE WA TANZANIA 8 MACHI, 2016

Tanzania ni mwanachama mwaminifu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki – Kutokana na milango kuwa wazi sasa Mheshimiwa Rais wetu Magufuli ametuhakikishia tunaweza kuvuka mipaka na kujitanua kupata fursa zaidi. Katika kuadhiminisha siku ya wanawake Duniani - Wanawake wa Tanzania tuinuke na tujihakikishie kushiriki kikamilifu katika ubunifu wa biashara endelevu ambazo zitakuwa na viwango vya kukidhi matakwa ya kijumuiya, tuache kutengeneza bidhaa za kuishi muda mfupi na zisizo na ubora. Fursa zinatutembelea tuwe wasomaji wa magazeti na vitabu hata mitandao ya kijamii ili tuweze kujipatia mbinu za kutengeneza na kuuza  bidhaa za aina mbalimbali ambazo ni za kwetu wenyewe na sio kuchat na kudadisi tu kupitia mitandao muda wote, tuitumie hii mitandao kwa manufaa ya kutangaza biashara zetu wenyewe. “HAPA KAZI TU”.

Tumehakikishiwa kwamba bidhaa za ndani sasa zimepewa kipaumbele, ebu tuamke na kukimbilia Taasisi za fedha kama vile CRDB, NMB, NBC, EXIM, BOA, POSTA, FINCA, BLACK na BLUE na Taasisi zingine za fedha kuweza kuchukua mikopo yenye tija kwa uzalishaji wa uhakika.  Wanawake tunaweza sana, tuache hofu na uoga wa kushindwa.  “Sikuzote  asiyekubali kushindwa sio mshindani”.

Maisha ili yawe mepesi wanawake  tunatakiwa tujitoe kwa hali na mali, kinamama tuwe mfano kwa kizazi kijacho kwa kujihakikishia tumejipanga kufika mbali katika biashara zetu ili kuinua uchumi wetu na familia zetu. Tukifanya biashara zetu sisi ndio tutakaoweza kuwaandalia watoto wetu maisha mema na yenye tija. Tunaweza kuchangia madawati, madaftari na vitabu vya kiada vya watoto na huduma nyingine nyingi katika jamii yetu. Kwani ukimwelimisha mwanamke umeielimisha jamii nzima na pia kila mwanaume aliyefanikiwa nyuma yake kuna mwanamke.  Tunalilia usawa basi na tukimbilie fursa kwa usawa.

Tanzania wanawake ni wengi sana hasa wafanyakazi na wafanyabiashara, kwa wale waliofanikiwa tuwafundishe wengine mbinu za kuweza kujiinua kwa urahisi na kufikia malengo. Maarifa ukimgawia mwingine unafanikiwa zaidi tuondoe ile hari ya wivu na masengenyo wakati wote sisi kwa sisi.  Tuwe tayari kuwauliza wanawake waliofanikiwa njia gani wamepita au wanapitia ili tuweze kujifunza kupitia wao.  Wanawake tuwe wazuri katika kurejesha mikopo katika Taasisi za fedha kwani wanawake wengi wanakopa na kukimbilia Taasisi nyingine na kuacha madeni yasiyolipika. Mafanikio hayakimbiwi ila mafanikio yanakimbiliwa.

Naamini ujumbe huu utawafikia wanawake wa Tanzania nzima ili tuamke na kuchangamkia fursa zozote zinazojitokeza kwa kipindi hiki cha “HAPA KAZI TU” kwani asiyefanya kazi na asile.

Wanawake tunaweza.

Lusako Mwakiluma
MKURUGENZI WEZESHA TRUST FUND


 
Copyright © 2013 WEZESHA TRUST FUND
Powered by WordPress24x7