Wezesha Trust Fund imetimiza miaka minne tangu kuanzishwa Agosti,
2016 kwa kuwa karibu na Jamii
inayoizunguka kama vile Hospitali ya Sabasaba iliyoko katika kata ya Mafiga na
Uwanja wa Taifa, nia na madhumuni ni kuonyesha mfano kwa jamii kwamba
tunatakiwa tufanye usafi katika maeneo yetu bila shuruti tukiamini usafi
unaanzia nyumbani.
Wezesha ofisi zake ziko Kata ya Uwanja wa Taifa, pia Wezesha ni
Asasi ya kijamii ambayo inafanya kazi pamoja na wanajamii na kupitia kazi
hizo kunaifanya Wezesha kujua matatizo ya jamii inayoizunguka na kuweza
kuyatatua yale yaliyo ndani ya uwezo na yale yaliyo nje kuyapeleka kwa Serikali
- Kiwilaya na Kimkoa ili kuweza kuyapatia ufumbuzi wa kina.
Pia iliandaa Bonanza kubwa la Mpira wa Miguu na kuinua vipaji kwa
vijana katika muziki, kuimba na kucheza ili kuweza kuwapeleka mbele zaidi.
Mechi kati ya Mawenzi Market na Polisi Moro ilichezwa na makusanyo ya kiingilio
kilichopatikana yalienda kusaidia kufanya utafiti kwa waishio katika
mazingira magumu wanaofanya shughuli zao Mawenzi Sokoni na nyingine
zitawaandalia stadi za kazi baadhi ya watoto walio chini ya umri wa miaka kumi
na nane(18) na wale wakurudi shuleni chini ya umri wa miaka (18) watarudishwa
kwa mujibu wa sheria.
Wafanyakazi wa Wezesha Trust Fund wakifanya usafi katika Hospitali ya Saba-Saba Mkoani Morogoro katika kuadhimisha siku ya WEZESHA DAY - AGOSTI, 2016. Tukianzia na kushoto ni Mkurugenzi Bi Lusako Mwakiluma, Abubakari Mkingiye, Mohamedi Nyongo, John Ndumbalo, Wellingtone Maselle na Salum Tindwa.
Tunakwenda sambamba na Kauli mbiu ya Rais wetu Mheshimiwa Dr John Pombe Magufuli.
Hapa Kazi tu!!!
Lusako Mwakiluma
Mkurugenzi
Wezesha Trust Fund
Kauli Mbiu - "Wakiwezeshwa wanaweza"
Post a Comment