Fursa za wanawake ziko nyingi sana lakini wanawake wenyewe
hawana motisha ya kuzikimbilia na kwenye uzalishaji mali wako vizuri sana ila
tu kuna baadhi ya wanawake ni waoga kujaribu nab ado wanaamini kuwa mwanaume ni
mtafutaji na mwanamke ni mama wa nyumbani siku zote. Hii inaonyesha mwanamke akiishi bila
mume au akikimbiwa na mwanaume
anashindwa kusimama kwa hofu ya
kushindwa maisha. Kuna fursa za
kibiashara, ufugaji na utengenezaji bidhaa mbalimbali ambazo kila siku
zinajitokeza lakini katika suala la kujifunza wanawake ni wazito na hata
kuuliza kama kitu hawawezi pia ni taabu.
Wezesha Trust Fund inatumia njia nyingi
katika kuwaelimisha wanawake: Inatumia
Television, Redio, semina na warsha za mara kwa mara. Wanawake wengi wanatambua kuwa kila mwanaume aliyefanikiwa
nyuma yake yuko mwanamke na ukikuta mwanamke kafanikiwa ujue nyuma yake yuko
peke yake. Wanawake pia wana majukumu mengi ya kifamilia na ya kibiashara, apike, afue, aende kazini, anyonyeshe na pia amhudumie mume na watoto. Muda wake ni ule ule na kazi ni nyingi, kuna muda anachoka kwani naye ni binadamu.
Wakati naongea na wanawake hawa nakutana na
changamoto nyingi wanazopitia wanalalamika wenyewe kwamba hawajiamini, waoga,
na wakiona biashara kidogo zinasumbua wanaacha.
Na kuna wengine mitaji inakata kwa sababu ya waume zao wanawaachia
majukumu ya nyumbani na pia wanaume hao hao hawawapi fursa wanawake zao za
kufanya biashara kwa upana zaidi. Pia wengine wanawakataza wasitoke majumbani
kwenda kwenye biashara. Wapo wanawake
wengine wao makundi yanawaharibu wanaishi maisha ya kuiga na kutamani vitu nje
ya uwezo wao.
Ushauri wangu adui wa mwanamke ni yeye
mwenyewe na pia kutokana na mfumo uliopo
tangu awali wanawake ni viumbe hafifu na
wengi wanafahamu hivyo na hawataki kuchukua hatua, wainuke na waseme hapana
inapobidi kusema hapana. Wanaume nao nawaomba waache kuwakatisha tamaa wake
zao bali wawatie moyo kwani wanawake
wakitiwa moyo na nguvu wana ujasiri kuliko hata wanaume, pia kuna wakati wawasaidie majukumu ya nyumbani kama yanakuwa mengi. Pia wanawake ni wazuri katika kutunza fedha. Nawaomba wanawake wenzangu wajidhatiti katika
kusimamia kile walichonacho ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea ya
maendeleo.
Wezesha na wadau wengine
hatutaacha kuwatia moyo wakati wote watakapohitaji ushauri wa kitaalamu. Kauli Mbiu yetu siku zote: “Wakiwezeshwa wanaweza”
Karibuni
tulishirikiane kulijenga Taifa letu kwa bidii na maarifa.
Lusako
Mwakiluma
Mhamasishaji
na muinuaji waliokata tamaa
Post a Comment