Kwa nini
unataka kuwa na pesa nyingi, je pesa nyingi zitakupatia amani au furaha?
Kuwa na pesa
nyingi itakupatia amani. Kama utakuwa
na pesa nyingi utalipa madeni yako yote,
utakwenda popote unapotaka kwenda na utafanya chochote unachotaka kufanya.
Ninachotaka
kukufahamisha hapa ni kwamba kuwa na
pesa nyingi itakusaidia kuponya vitu
vyote? Usije ukaanguka mwenyewe kwenye
eneo la kufikiria. Kama unafikiria pesa itakupatia furaha, utakuwa unajidanganya
mwenyewe.
Hauwezi kuwa
na furaha utakapokuwa na pesa nyingi labda unaweza kuwa na furaha usipokuwa na
pesa. Kama ni mtu mwenye kumaanisha,
kuwa tajiri kutakufanya uwe na uhuru wa kujiamulia mambo yako mwenyewe kwa kile
ulichonacho kwa wakati ule. Kama utakuwa
mtu mwenye huzuni, kuwa tajiri utakuwa
umejipa uhuru wa kuitafuta furaha yako kwa wakati huo.
Kuwa tajiri
ni kwamba tayari umeshaandaa kiasi cha pesa ambacho ulikitafuta. Ufahamu wako utakuwa unajihakikishia kuwa mtu
ambaye hapo mwanzo haukuwa hivyo na cha muhimu ni kuvunja sheria ya kujipangia
matumizi yako ya pesa kabla ya kuishika mkononi.
Mfano: 30% kwa ajili ya matumizi ya kuishi
30% kwa ajili ya matumizi ya
kuweka akiba
30% kwa ajili ya matumizi ya
starehe na furaha ya familia
10% kwa ajili ya kuwapatia
wasionacho
Asilimia mia
moja (100%) ya kila pesa yako igawanye katika mafungu manne.
Kitu cha
muhimu sana ni kufanya kazi kwa bidii yako mwenyewe kuliko kufanya kazi kwa
ajili ya kutafuta utajiri. Ni muhimu
kufanya hivyo kwasababu kiasi cha utajiri
wa mtu alichonacho hakiwezi kuzidi
maendeleo yake binafsi.
Ngoja nikupe
mfano: Ni mara ngapi unasikia mtu
ameshinda bahati nasibu na amepata kiasi kikubwa cha pesa? Halafu baada ya muda mfupi unasikia zile pesa
zote zimeisha kwa muda mfupi sana.
Kumbuka
alikuwa anasema kabla ya kuzipata pesa hizo.
Kama nikishinda kiasi kikubwa cha pesa kwenye bahati nasibu nitafanya
kitu kikubwa na nitakuwa tajiri mkubwa sana, kumbuka alisema wakati hajazishika
hata wewe wakati hauko na pesa unasema nikizipata. Je, umepanga chochote kabla ya hizo pesa
kupatikana au utapanga ukishazipata? Utafiti unaonyesha kwamba bahati nasibu ni
kitu kinachojulikana sana na watu wanaamini katika bahati nasibu kwa sababu
mbili:
1. Mpango wa pesa za haraka haraka
2. Pia ni mchezo wa furaha
Ni mchezo
unaochezwa kila siku leo unaweka pesa kidogo na kesho unapata kiasi kikubwa
basi ni kitu endelevu na watu wanategemea kuna siku nitapata zaidi ya jana. Hii inakuhakikishia kama utapata basi
utamaliza shida zako zote. Na yale yaliyosimama yote yatafanikiwa kwa urahisi.
Watu wengi wanaandaa kesho yao kwa kujinyima leo ili kesho yao iwe nzuri zaidi.
Hauwezi kuwa
tajiri mpaka uvunje sheria kwa kujihakikishia kila pesa yako unayoipata
unaivunja mara nne ili uweze kutimiza azma yako uliyojiwekea. Nitakuletea
mpango mzima wa kuwa tajiri kwa haraka kwa kuvunja sheria.
Karibu sana
tuchangie hoja, tutoe maoni na tujihakikishie kufika pale tunapopataka.
Lusako
Mwakiluma
Mhamasishaji
na Muinuaji kwa waliokata tama
Wezesha
Trust Fund - Morogoro
26 Desemba, 2016
Post a Comment