1. Chagua watu wenye ujasiri na wenye hari
ya chanya ndani yake
Kaa na watu wenye ujasiri, ukikaa na
watu wenye ujasiri nawe utakuwa jasiri kwani utajifunza kupitia wao kumbuka
hata Biblia inasema enenda na wenye hakima nawe utakuwa na hekima mithali 13:20
lakini rafiki wa wapumbavu atahangamia.
2. Fanya kila siku kitu kinachokufurahisha
au kukifurahia.
Ukifanya
kitu ambacho haupendi kufanya hauwezi kutunza ujasiri wako, utakuwa unafanya
huku haujiamini. Fanya kile kitu roho
yako inataka na utaona unakifanya katika hari kuu na kubwa sana.
3. Zingatia malengo na mipango
uliyojiwekea
Malengo ni muhimu sana katika maisha ya
kila binadamu. Kama hauna malengo basi
amini kwamba ufahamu wako umekufa.
Malengo na mipango yako ndiyo inayokupelekea kufika mbali kimaisha. Hauwezi kufanya mambo kiholelaholela. Mipango ndiyo matumizi yako ya kila siku. Mipango na malengo ni dira ya mafanikio
yako. Andika kwenye daftari au kitabu
malengo yako kisha uyafanye kwa mpangilio unaoutaka kwa muda uliojiwekea.
4. Usikate tamaa
Katika safari ya maisha hakuna kukata tamaa
na mtu jasiri hakubali kushindwa kwa lolote.
Hivyo hata kama unaona kuna kushindwa usikate tama kabisa. Songa mbele uweze kuiona siku nyingine na
mwisho kufikia malengo uliyojiwekea.
5. Tumia muda wako vizuri
Muda ni pesa, na wakati ni mali masaa 24
tuliyopewa na mwenyezi Mungu wote tunayo.
Iweje tajiri afanikiwe kwa masaa haya haya 24 na wewe ushindwe katika
masaa haya 24 inabidi ujiangalie tena na tena.
Pia usiogope kujaribu kwa kuhofia kushindwa kwa muda uliopo, unaweza
ukashindwa kumbe ndiyo ushindi wako unapoanzia.
Karibu sana tuendelee kuinuana na
kutiana nguvu.
Lusako
Mwakiluma
(Motivational & Inspirational
speaker)
Post a Comment