Kwa nini
leo nimefikiria haya? Naomba nikwambie
pesa ni jawabu la mambo yote namadhambi yote yameanzia kwenye pesa. Unaweza kuwa na rafiki au ndugu mliyeshibana
sana lakini pesa ikaja kuwatenganisha kwa urahisi mno na mkachukiana
milele. Pesa inatengeza marafiki na pia
inaleta uadui ndani yake. Basi ili uishi
kwa amani kila kitu unatakiwa ukifanye kwa kiasi.
Kila
wakati fanya msaada wa kipesa kama zawadi usifanye kama mkopo. Kama haujampa mtu msaada wa kipesa urafiki wenu unaenda kuisha
taratibu. Kama uko kwenye eneo la kuweza kumsaidia mtu basi msaidie usimkopeshe
mpe tu. Na kama unajua hauwezi kumpa
usimkopeshe itaenda kukuumiza wewe mwenyewe
(Ron Henley).
Sababu
ya kutompatia mkopo rafiki au ndugu wa karibu ni kwasababu ya kuondoa usumbufu
usio wa lazima wa kudaiana pasipo mashiko. Uhusiano wenu unaenda kuvunjika kama
sio kuharibika kabisa. Sababu ya watu
inayowapelekea kupata matatizo ya kipesa ni kutojua jinsi ya kufanya kazi na pesa
au jinsi ya kutumia fedha. Ukiwakopesha
wala hawajui wanaenda kufanyia nini kwani hawajajiandaa cha kwenda kufanyia
hizo pesa.
Kabla
ya kufahamu hivyo watachukua pesa kwako tena wataanza kutoa udhuru wa kushindwa
kukurudishia. Kinachofuata hapo ni
kukukimbia kila wanapokuona. Kuacha
kupokea simu yako na mwisho kutofungua mlango mara unapopiga hodi majumbani
kwao.
Naomba
kwa ushauri kama unataka kumsaidia ndugu yako au rafiki mpatie pesa kama msaada
na sio mkopo ili uishi kwa amani kwani utakapomkopesha hiyo pesa usiihesabu
katika akiba yako kwani imeondoka na hauwezi fahamu itarudi lini.
Hii ni
kwa faida yako ya watu wengine.
Karibu tusaidiane
pale tuliposhindwa na tunapoweza tuelekezane.
Kwani
maarifa ni mali kuliko pesa.
Lusako
Mwakiluma
Mhamasishaji
na Muinuaji kwa waliokata tamaa na kuugua
27 Desemba,
2016
Post a Comment