Wezesha Trust Fund & Victory Youth Support Organization kwa pamoja wamefanya kongamano la vijana waishio katika mazingira magumu Mkoani Morogoro lenye dhima "KIJANA JITAMBUE KUNA FURSA MBELE YAKO" kongamano lilifanyika katika Ukumbi wa UNGO(Umoja wa Asasi sizizo za kiserikali) Jengo la CCM Mkoa wa Morogoro. Vijana arobaini na 48 walihudhuria na wamejifunza mambo mengi yenye maana katika maisha yao kati ya vitu walivyojifunza kwenye kongamano:-
- Jinsi ya kijana kujitambua
- Jinsi ya kubadilisha unavyofikiria kama kijana wa leo na kufungua macho
- Mikakati iliyoandaliwa kuwaletea vijana maendeleo Mkoani Morogoro
- Mikakati iliyowekwa na kuonyesha fursa kwa vijana kama mikopo, kuboresha elimu zao, mbinu za kuwainua kiuchumi, kuwapatia ajira wasio na ajira na fursa nyingine nyingi kutegemea na kijana yuko wapi na anataka nini kwa wakati huo.
Picha
za vijana waliohudhuria pamoja na waandishi wa habari
Picha
ya Mkurugenzi wa Wezesha Trust Fund Bi Lusako Mwakiluma akitoa mada ya elimu ya utambuzi kwa vijana
wajitambue na kujua thamani yao kabla ya kupata fursa
Mkurugenzi
wa Victory Youth Support Organisation Bw. Freddy Ng'atigwa akielimisha vijana fursa zilizopo
na jinsi ya kuzipata
Post a Comment