Kwa sababu
tumeumbwa tofauti, wako walioumbwa kushughulika na mambo ya wenzao tu muda wote
wanaangalia fulani kafanya nini na kafanikiwa au kashindwa kwa kiasi gani. Mwisho wa siku ukiwaangalia watu hawa
utajikuta unashindwa kufikia malengo yako na kukwama njiani katika safari yako
ya maisha. Ndugu yangu simama katika
nafasi yako na usiwaangalie walioshindwa, walioshindwa wana maneno mengi
sana. Na ukiwafuata watakupotezea dira
kabisa. Amini kile unachokifanya na
amini kwamba kitafanikiwa kwa asilimia mia moja pamoja na hali zilizopo usirudi
nyuma Mungu ni mwema kwetu siku zote na yeye anaangalia mwisho wako sio mwanzo
wako.
Kuna watu
wameumizwa, kuna watu wameachwa, kuna watu wamekimbiwa na kuna watu wamefiwa na
kukataliwa na kuonekana si kitu kwenye jamii zao zinazowazunguka. Nakuomba ndugu yangu usifikirie kujiua au
kususa kwa ajili ya maisha yako simama ukijipa moyo kwamba wewe sio wa kwanza
unayepitia haya mama yangu nimpendaye sana Maya
Angelou mwandishi wa vitabu na misemo yake mizuri alisema katika mahojiano
yake na Oprah Winfrey “kwamba kila unachopitia amini sio wa kwanza kukipitia
wapo waliopitia unayopitia tafuta njia mbadala na kisha endelea mbele”
nakwambia muda sio wetu hata kwa kuuza maji ya mia mia utatoka tu. Usikae chini na kukata tamaa utapoteza dira
yako.
Hayo
yaliyopita chukulia kama changamoto na hao waliokuacha na kukumbia wachukulie
kama ngazi ya kupandia kuelekea kwenye mafanikio yako na yachukulie ya jana
kama historia ya kuja kuwashuhudia watu waliokuwa na hali kama hizo kwa
baadae. Amina tu na songa mbele kwani
adui ni ngazi ya kupandia na unaombwa kila siku kumpenda adui yako, jiulize je.,
huyu adui yangu akifa huyu nani atakuja kunipigia makofi wakati naenda
kufanikiwa na kuwashuhudia wengine nilikotoka?.
Kuwa na roho ya unyenyekevu na ya msamaha kwa yeyote anayekwenda kinyume
na wewe kwani hakuna barabara ndefu bila kona na hakuna yaliyo marefu bila kuwa
na ncha. Kumbuka kwa wale wakristo
Danieli, Meshack na Abelnego waliwekwa kwenye tanuru na hawakuungua kwa sababu
ya imani ya Mungu wao waliyemwamwini kwanini usiwe wewe ule moto ni changamoto
kama hizi ninazokuhadithia hapa. Naamini
kuna watu wanaenda kupokea miujiza yao ya mafanikio kupitia changamoto hizi za
maisha nasema maisha ni rahisi kama unayapatia na ni magumu kama unapoteza muda
kuangalia tatizo badala la suluhisho la tatizo lako. Jiulize Bill Gates, Obama, Hillary Clinton
wao wamezaliwa na nani na wananguvu gani za kukushinda wewe ambaye una masaa hayo
hayo na nguvu kama zao. Inuka twende
mbele tusipoteze muda wala saa.
Nakutakia
usomaji mwema wa mada zangu na Mungu atakuinua kwa namna ya tofauti
mpendwa.
Karibu
sana
Lusako
Mwakiluma
Post a Comment