BREAKING NEWS

VIDEO

BIASHARA

USHAURI WETU

Tuesday, December 27, 2016

WEZESHA TRUST FUND - MOROGORO YAFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA

WEZESHA TRUST FUND WALIPOTEMBELEA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA CHA BIGWA - MGOLOLE
TAREHE 26/12/2016. 
WALITOA MISAADA  MBALIMBALI KUSHEREHEKEA SIKU YA KUFUNGUA ZAWADI 
 PAMOJA NA WATOTO HAO   
WALITOA MISAADA YA SAMAKI, NYAMA, MATUNDA, SABUNI, SUKARI NA VINYWAJI MBALIMBALI  


Wafanyakazi wa Wezesha Trust Fund - Morogoro wakisaini kitabu cha Wageni Bigwa Mgolole - Kituo cha kulelea watoto yatima kutoka kushoto Mkurugenzi Bi Lusako Mwakiluma, Daktari Dr Elias Yuda Mtungilwa, Msaidizi wa Utawala na Mwalimu wa Tehama Maines Richard, Afisa Mafunzo Mohamed Nyongo.

Wezesha Trust Fund wakifurahi pamoja na  Sista mlezi pamojawatoto yatima mara baada ya kukabidhi misaada, watoto walifurahi sana kupokea zawadi zao.

Wafanyakazi wa Wezesha Trust Fund wakiwabembeleza watoto yatima ambao ni wachanga wanaolelewa katika kituo hicho, 

 Wezesha Trust Fund kwa pamoja inaiomba jamii kuwa na tabia ya kuangalia watoto kama hawa katika vituo vilivyo karibu na mbali kwani ni faraja kubwa kuhakikisha yatima wanapata furaha kama watoto wengine.  Yatima ni watoto wetu tusiwatenge wala kuwabagua.
Wezesha Trust Fund wakiwa pamoja na watoto yatima wa darasa la kwanza na pili - kituoni hapo wakiongozwa na Derick na David(mapacha) ambao tangu wakiwa na siku tatu baada ya kuzaliwa na kufiwa na mama yao Wezesha inawatembelea na kila wanapowaona wafanyakazi wa Wezesha wanafurahi sana.
Mungu wabariki walezi wa watoto hawa yaani Masista wote wanaohusika na pia wabariki watoto yatima wote wakue katika maadili mema na kumtegemea Mungu.

Sunday, December 25, 2016

USIMKOPESHE RAFIKI AU NDUGU YAKO

Kwa nini leo nimefikiria haya?  Naomba nikwambie pesa ni jawabu la mambo yote namadhambi yote yameanzia kwenye pesa.   Unaweza kuwa na rafiki au ndugu mliyeshibana sana lakini pesa ikaja kuwatenganisha kwa urahisi mno na mkachukiana milele.  Pesa inatengeza marafiki na pia inaleta uadui ndani yake.  Basi ili uishi kwa amani kila kitu unatakiwa ukifanye kwa kiasi. 

Kila wakati fanya msaada wa kipesa kama zawadi usifanye kama mkopo.  Kama haujampa mtu  msaada wa kipesa urafiki wenu unaenda kuisha taratibu. Kama uko kwenye eneo la kuweza kumsaidia mtu basi msaidie usimkopeshe mpe tu.  Na kama unajua hauwezi kumpa usimkopeshe itaenda kukuumiza wewe mwenyewe
(Ron Henley).

Sababu ya kutompatia mkopo rafiki au ndugu wa karibu ni kwasababu ya kuondoa usumbufu usio wa lazima wa kudaiana pasipo mashiko. Uhusiano wenu unaenda kuvunjika kama sio kuharibika kabisa.  Sababu ya watu inayowapelekea kupata matatizo ya kipesa ni kutojua jinsi ya kufanya kazi na pesa au jinsi ya kutumia fedha.  Ukiwakopesha wala hawajui wanaenda kufanyia nini kwani hawajajiandaa cha kwenda kufanyia hizo pesa. 
Kabla ya kufahamu hivyo watachukua pesa kwako tena wataanza kutoa udhuru wa kushindwa kukurudishia.  Kinachofuata hapo ni kukukimbia kila wanapokuona.  Kuacha kupokea simu yako na mwisho kutofungua mlango mara unapopiga hodi majumbani kwao.

Naomba kwa ushauri kama unataka kumsaidia ndugu yako au rafiki mpatie pesa kama msaada na sio mkopo ili uishi kwa amani kwani utakapomkopesha hiyo pesa usiihesabu katika akiba yako kwani imeondoka na hauwezi fahamu itarudi lini. 
Hii ni kwa faida yako ya watu wengine.

Karibu tusaidiane pale tuliposhindwa na tunapoweza tuelekezane.

Kwani maarifa ni mali kuliko pesa.

Lusako Mwakiluma
Mhamasishaji na Muinuaji kwa waliokata tamaa na kuugua

27 Desemba, 2016

JE, KUWA TAJIRI KUTAKULETEA FURAHA

Kwa nini unataka kuwa na pesa nyingi, je pesa nyingi zitakupatia amani au furaha? 
Kuwa na pesa nyingi itakupatia amani.   Kama utakuwa na pesa nyingi  utalipa madeni yako yote, utakwenda popote unapotaka kwenda na utafanya chochote unachotaka kufanya.

Ninachotaka kukufahamisha  hapa ni kwamba kuwa na pesa nyingi itakusaidia  kuponya vitu vyote?  Usije ukaanguka mwenyewe kwenye eneo la kufikiria. Kama unafikiria pesa itakupatia furaha, utakuwa unajidanganya mwenyewe.

Hauwezi kuwa na furaha utakapokuwa na pesa nyingi labda unaweza kuwa na furaha usipokuwa na pesa.  Kama ni mtu mwenye kumaanisha, kuwa tajiri kutakufanya uwe na uhuru wa kujiamulia mambo yako mwenyewe kwa kile ulichonacho kwa wakati ule.  Kama utakuwa mtu mwenye huzuni, kuwa tajiri utakuwa  umejipa uhuru wa kuitafuta furaha yako kwa wakati huo.

Kuwa tajiri ni kwamba tayari umeshaandaa kiasi cha pesa ambacho ulikitafuta.  Ufahamu wako utakuwa unajihakikishia kuwa mtu ambaye hapo mwanzo haukuwa hivyo na cha muhimu ni kuvunja sheria ya kujipangia matumizi yako ya pesa kabla ya kuishika mkononi.
Mfano:   30% kwa ajili ya matumizi ya kuishi
                30% kwa ajili ya matumizi ya kuweka akiba
                30% kwa ajili ya matumizi ya starehe na furaha ya  familia
                10% kwa ajili ya kuwapatia wasionacho
Asilimia mia moja (100%) ya kila pesa yako igawanye katika mafungu manne.

Kitu cha muhimu sana ni kufanya kazi kwa bidii yako mwenyewe kuliko kufanya kazi kwa ajili ya kutafuta utajiri.  Ni muhimu kufanya hivyo kwasababu kiasi cha utajiri  wa mtu alichonacho hakiwezi kuzidi  maendeleo yake binafsi.
Ngoja nikupe mfano:  Ni mara ngapi unasikia mtu ameshinda bahati nasibu na amepata kiasi kikubwa cha pesa?  Halafu baada ya muda mfupi unasikia zile pesa zote zimeisha kwa muda mfupi sana.

Kumbuka alikuwa anasema kabla ya kuzipata pesa hizo.  Kama nikishinda kiasi kikubwa cha pesa kwenye bahati nasibu nitafanya kitu kikubwa na nitakuwa tajiri mkubwa sana, kumbuka alisema wakati hajazishika hata wewe wakati hauko na pesa unasema nikizipata.  Je, umepanga chochote kabla ya hizo pesa kupatikana au utapanga ukishazipata? Utafiti unaonyesha kwamba bahati nasibu ni kitu kinachojulikana sana na watu wanaamini katika bahati nasibu kwa sababu mbili:
            1. Mpango wa pesa za haraka haraka
            2. Pia ni mchezo wa furaha

Ni mchezo unaochezwa kila siku leo unaweka pesa kidogo na kesho unapata kiasi kikubwa basi ni kitu endelevu na watu wanategemea kuna siku nitapata zaidi ya jana.  Hii inakuhakikishia kama utapata basi utamaliza shida zako zote. Na yale yaliyosimama yote yatafanikiwa kwa urahisi. Watu wengi wanaandaa kesho yao kwa kujinyima leo ili kesho yao iwe nzuri zaidi.

Hauwezi kuwa tajiri mpaka uvunje sheria kwa kujihakikishia kila pesa yako unayoipata unaivunja mara nne ili uweze kutimiza azma yako uliyojiwekea. Nitakuletea mpango mzima wa kuwa tajiri kwa haraka kwa kuvunja sheria.

Karibu sana tuchangie hoja, tutoe maoni na tujihakikishie kufika pale tunapopataka.

Lusako Mwakiluma
Mhamasishaji na Muinuaji kwa waliokata tama
Wezesha Trust Fund - Morogoro

26 Desemba, 2016


Sunday, December 11, 2016

FORTUNE TEAM WAKIFANYA USAFI SABASABA HOSPITAL - MOROGORO


Wezesha Trust Fund wakiwafundisha kazi za kujitolea Fortune Team kutoka shule ya sekondari Uwanja wa Taifa siku ya 1 Desemba, 2016 kuazimisha siku ya Ukimwi Duniani, Timu ya Fortune inafahamu jinsi ya kusema hapana na kujikinga na VVU/Ukimwi wakiamini Vijana bila ukimwi inawezekana.

Fortune Team wakiendelea na kufanya usafi kwa kujitolea kama walivyofundishwa na Wafanyakazi wa Wezesha Trust Fund - Morogoro
Fortune Team wakiendelea na usafi baada ya kuhitimisha mafunzo yao ya siku Moja ya kuepuka na kujikinga na Ukimwi mashuleni.

Mkurugenzi wa Wezesha akihakikisha kwamba usafi unafanyika kwa kiwango cha hali ya juu katika Hospitali ya Sabasaba ndani ya kata ya Uwanja wa Ndege.


 Mohamedi Nyongo afisa  Mafunzo akishirikiana na Fortune Team kufanya usafi kwani mtoto umleavyo ndivyo akuavyo na mifano ni lazima kwa wanafortune team.  Mungu ibariki Wezesha na Mungu ibariki Fortune Team.
 Mkurugenzi wa Wezesha Trust Fund akihojiwa na Vyombo vya habari kuhusiana na siku hiyo.  East Africa Radio na Television walikuwepo pia SUA Television walisimama kidete kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa sawa.
Afisa Tawala Bi Mainess Derick akiwa pamoja na Fortune Team kwa msisitizo wa siku ya Ukimwi Duniani wakiamini kuwa maombukizi mapya ya Ukimwi kutoongezeka na kuhakikisha yanapungua kama sio kumalizika.

Ilikuwa ni siku ya Ukimwi Duniani 1 Desemba, 2016

Fortune Team ni wanafunzi toka Shule ya Sekondari Uwanja wa Taifa waliojiunga na Wezesha Trust Fund kama mabalozi wa wanafunzi wengine katika kuhakikisha wanafuata maadili ambayo nao wamefundishwa na kuelimishwa na Wezesha Trust Fund - Morogoro ikiwa ni muendelezo wa kazi ya kuwaelimisha Vijana rika kuweza kufanikiwa katika malengo yao waliyojiwekea kwa kuepuka vishawishi toka kwa wanawake na wanaume, mimba na ndoa za utotoni, Semina ilifanyika tarehe 19/11/2016 katika Ukumbi wa Pastor Phil Training Centre.

Mambo matano waliyojifunza:

1. Elimu ya Kujitambua
2. Jinsi ya kuepuka mimba na ndoa za utotoni
3. Elimu ya Ukimwi na VVU na jinsi ya kuepuka
4. Jinsi ya kusoma na kufaulu kwa kiwango cha juu
5. Elimu ya kufanya kazi za kujitolea

Wezesha pia inawashukuru Viongozi wa Mkoa wa Morogoro kwa ushirikiano wa siku hii ya usafi kwani ilikuwa ni kuwafundisha vijana hawa kufanya kazi ya kujitolea katika jamii kwa hiari yao.  Tunashukuru Mkurugenzi wa Manispaa, Mganga Mkuu wa Mkoa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sabasaba kwa ushirikiano waliotupatia.  Tunasema asante sana.  Kauli mbiu ya siku ya tarehe 1 Desemba, 2016 saidia kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi. 

BOFYA HAPA KUONA TUKIO LA SIKU YA WEZESHA

NJIA TANO ZA KUONGEZA UJASIRI WAKO

1.   Chagua watu wenye ujasiri na wenye hari ya chanya ndani yake
Kaa na watu wenye ujasiri, ukikaa na watu wenye ujasiri nawe utakuwa jasiri kwani utajifunza kupitia wao kumbuka hata Biblia inasema enenda na wenye hakima nawe utakuwa na hekima mithali 13:20 lakini rafiki wa wapumbavu atahangamia.

2.     Fanya kila siku kitu kinachokufurahisha au kukifurahia. 
Ukifanya kitu ambacho haupendi kufanya hauwezi kutunza ujasiri wako, utakuwa unafanya huku haujiamini.  Fanya kile kitu roho yako inataka na utaona unakifanya katika hari kuu na kubwa sana.

3.     Zingatia malengo na mipango uliyojiwekea
Malengo ni muhimu sana katika maisha ya kila binadamu.  Kama hauna malengo basi amini kwamba ufahamu wako umekufa.  Malengo na mipango yako ndiyo inayokupelekea kufika mbali kimaisha.  Hauwezi kufanya mambo kiholelaholela.  Mipango ndiyo matumizi yako ya kila siku.  Mipango na malengo ni dira ya mafanikio yako.  Andika kwenye daftari au kitabu malengo yako kisha uyafanye kwa mpangilio unaoutaka kwa muda uliojiwekea.

4.     Usikate tamaa
Katika safari ya maisha hakuna kukata tamaa na mtu jasiri hakubali kushindwa kwa lolote.  Hivyo hata kama unaona kuna kushindwa usikate tama kabisa.  Songa mbele uweze kuiona siku nyingine na mwisho kufikia malengo uliyojiwekea.

5.     Tumia muda wako vizuri
Muda ni pesa, na wakati ni mali masaa 24 tuliyopewa na mwenyezi Mungu wote tunayo.  Iweje tajiri afanikiwe kwa masaa haya haya 24 na wewe ushindwe katika masaa haya 24 inabidi ujiangalie tena na tena.  Pia usiogope kujaribu kwa kuhofia kushindwa kwa muda uliopo, unaweza ukashindwa kumbe ndiyo ushindi wako unapoanzia. 

Karibu sana tuendelee kuinuana na kutiana nguvu.

Lusako Mwakiluma
            (Motivational & Inspirational speaker)
                 


BOFYA KUPATA HABARI YA KUMJALI MTEJA

 
Copyright © 2013 WEZESHA TRUST FUND
Powered by WordPress24x7